Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeihamishia Benki M Tanzania PLC
kwenda Azania Benki limited baada ya kubaini kuwa na upungufu wa ukwasi na
kutoa huduma kwa wateja.
Akizungumza Jijini Dar es
Salaam Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse alisema kuwa
Benki kuu imechukua uamuzi huo wa kuhamisha mali na madeni ya Benki M kwenda
Azani benki ili kuwezesha taasisi za kifedha kufanya kazi na kuwa imara zaidi
kwa kujifunza kupitia benki M.
“Kwa mamlaka iliyopewa
Benki Kuu ya Tanzania chini ya sheria kifungu 58(2) cha sheria za mabenki na
taasisi za fedha yay a mwaka 2006, Benki Kuu imeamua kuchukua jukumu hili ili
kuweza kulinda maslahi ya wateja wenye amana katika benki M Tanzania PLC”,
Alisema Gavana Msaidizi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse
Dkt. Kibesse alisema kuwa
kwa sasa Benki Kuu ya Tanzania, Azania Benki Limited na wadau wengine wa
taasisi za kifedha wako kwenye mchakato wa mwisho wa kisheria kuhusu
kukamilisha uhamishaji wa mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Benki Limited
na mchakato utakapokamilika Benki ya Azania utaujulisha umma kuhusu mchakato
huo.
Aidha Dkt. Kibesse
aliongeza kuwa mchakato huo hauendani na kusitishwa kwa marejesho ya mikopo kwa
wateja wa Benki M walioingia mkataba na kukopa kwenye benki ya kwamba wanapaswa
waendelee kurejesha mikopo hiyo na wanatakiwa kulipa ndani ya siku 7 tu.
“Wateja wote wenye mikopo
wanatakiwa waendelee kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao waliyoingia na
Benki M Tanzania PLC”, Alisisitiza Dkt. Kibesse.
Benki M ilianzishwa na
kupewa leseni ya shughuli za kibenki hapa Tanzania mwaka 2008 na ilikuwa moja
ya benki imara iliyokuza mtaji hadi kufikia fedha za kitanzania shilingi
trilioni 1 na kugawanyika katika matawi matano huku matawi makuu matatu yakiwa
Jijini Dar es Salaam na mengine Mwanza pamoja na Arusha matawi ambayo
yalilegalega mnamo mwaka 2018.
Tangu Tarehe 2 Agosti 2018
Benki Kuu ya Tanzania iliamua kuchukua jukumu la usimamizi kwa Benki M baada ya
kubaini benki hii kushindwa kulipa madeni yake ikiwemo amana za wateja wake,
pia Dkt.Kibesse amewahakikishia wadau wanaotumia huduma za kifedha kuwa Benki
Kuu ya Tanzania itaendelea kulinda maslahi yao pamoja na uhimilifu katika Sekta
ya Fedha nchini.
Post a Comment