Waziri Kamwele azindua meli ya DMI Seatim 1 ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam
Mwamba wa habari
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele amezindua Meli ya DMI Seatime 1 itakayotumiwa kwa mafunzo ya vitendo na Wanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam(DMI).
Meli hiyo ilitolewa na Mfanyabiashara Said Salim Bakharesa kwa chuo hicho ambapo baada ya kukabidhiwa ilifanyiwa ukarabati na Mkandarasi Songoro Marine.
Akizindua meli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya 14 ya Kilelee cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya chuo hicho Waziri Kamwele amesema dhumuni la kuifanyia ukarabati hadi kukamilika kwake imelenga kuwasaidia wanafunzi wa DMI wanaosomea taaluma za ubaharia na uinjinia wa meli kujifunza mazoezi ya vitendo.
" Chuo kilipewa meli hii na Bakhressa kikaanagalia jinsi gani ya kuifufua kwa kutumia gharama zake ina uwezo wa kubeba abiria 180 wa daraja la kwanza na pili," amesema Mhandisi Kamwele.
Amebainisha kuwa meli ifanyiwa majaribio na kwamba endapo itaonekana ina uwezo wa kuhimili mawimbi itatoa huduma ya usafiri kati ya Nyamisati-Mafia, Zanzibar na Tanga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa chuo hicho, Ernest Bupamba amesema kuwa ukarabati wa meli umegharimu Sh milioni 414.
Naye Kapteni Andrew amefafanua kuwa meli itaongozwa na Nahonda mkuu, msaidizi, Mhandisi mkuu na msaidizi wake pamoja na mtaalamu wa mafuta.
Post a Comment