Ads

UONGOZI WA YANGA WAMZUNGUMZIA M/KITI WA USAJILI NYIKA.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay ameshangazwa na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu yao juu ya kumshutumu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika kuhusiana na usajili.

Lukumay amesema baadhi yao wamefikia hatua ya kusema Nyika alimdanganya Kocha Zahera kuwa alimwahidi baadhi ya wachezaji lakini mwisho wa siku ikawa si kweli kama walivyokubaliana.

Kaimu Lukumay ameeleza ifikie hatua wapenzi wa Yanga waelewe klabu yao inapitia wakati gani hivi sasa kwani baadhi ya wachezaji aliowapendekeza Zahera dili zao zilikuwa kubwa na kuepelekea kushindwa kuwasajili.

Kiongozi huyo aliyekaimu nafasi hiyo kwa muda, ameshangazwa na lawama nyingi za wanayanga ambao hawajui klabu ipo kwenye hali mbaya kiuchumi kipindi hiki.

Yanga imefanikisha kunyaka saini mbili pekee za wachezaji katika dirisha ambao ni kipa Ibrahim Hamid na aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban

No comments