UONGOZI WA SOFAPAKA YA KENYA YATOA ONYO JAGWANI.
KASUMBA (KULIA) |
Mmoja wa viongozi wa Sofapaka ambaye amesema si msemaji wa klabu, amesisitiza, lolote sawa lakini tararibu zifuatwe.
“Naweza kukuambia wewe kwa kuwa ni rafiki yangu, kwanza si sawa kuona inazungumzwa mchezaji wako anatakiwa na wewe hujui lolote.
“Lakini sawa, kama wanamhitaji waje, tuwaeleze ofa yetu. Maana tumeelezwa huko Tanzania mnaandika tu kwamba anakuja kwenu huko Yanga,” alisema.
Hata hivyo, Yanga haijatamka zaidi ya kuwepo kwa fununu zinazoambatana na madalali wanaotaka kumleta mchezaji huyo nchini kuendelea kupiga debe.
Imeelezwa Kasumba ni mmoja wa wachezaji wazuri lakini wanaocheza kwa kufanana kabisa na Herietier Makambo.
Yanga imekuwa ikiendelea kutaka kujiimarisha katika ushambulizi wakati ikiendelea kuongoza ligi.
Post a Comment