TAASISI YA MARCUS MWEMEZI YATOA ELIMU JUU YA UGONJWA SONONA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM
Takwimu zinaonyesha kuwa mmoja kati watu wanne hapa nchini anatatizo la Sonona, Na Sonona ni ugonjwa unaoathiri watu wengi sana bila wao
wenyewe kujijua mpaka tatizo linapokuwa kubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Marcus Mwemezi Foundation Bi. Belinda Y. Nyapili akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema wiki hii katika semina za jinsia na maendeleo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Marcus Mwemezi Foundation Bi.
Belinda Y. Nyapili mapema wiki hii katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS)
wakati akiwasilisha mada ya athari za ukatili wa kijinsia katika afya ya akili.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Sonona ni ugonjwa wa akili ambao kwa kawaida umekuwa ukipewa majina mengi sana
kama Ukichaa, Uchizi, Utaira, Wendawazimu nk. Lakini pia dalili zake siyo za
moja kwa moja kama ugonjwa mwingine na inahitaji utashi wa hali ya juu kumgundua mtu anayeanza kuugua ugonjwa huu wa Sonona.
Aidha aliendelea
kusema kuwa visababishi vya ugonjwa huu ni vingi na vinategemea na wakati na
hali iliyomkuta mgonjwa, Na kuvitaja baadhi kuwa ni kuachishwa kazi, kuachwa na mpenzi wako, kufiwa na
mtu wa karibu aidha mke kufiwa na mumewe aliyempenda sana au mume kufiwa na
mkwe, Unyanyasaji wa kupita kiasi na mengineyo.
Aliongeza kuwa
Sonona ni ugonjwa ambao pia unaweza kusababisha mtu akajiua ama kujidhulu
endapo atafikiri kwa muda mrefu bila kupata majibu, Na kuendelea kusema kuwa dalili za mtu
menye maradhi haya ni kupenda kujitenga na watu ambao mwanzoni alikuwa
akichangamana nao, Kuwa na huzuni iliyopitiliza, Unywaji wa pombe kupita kiasi. Na endapo utaona kuna ndugu
yako au mtu wako wa karibu anadalili hizo unaweza kuonana na wataalamu wa Saikolojia kwa
msaada zaidi.
Mwanaharakati Nyanjura Kalindo Akichangia mada katika Semina ya Jinsia na Maendeleo mapema wiki hii.
Kwa upande
wake Mwanaharakati Nyanjura Kalindo
alisema kuwa ukatili wa kijinsia katika Nyanja ya uchumi inaweza kuwa ni
kisababishi kikubwa cha ugonjwa huu na kuwataka watanzania kuvunja ukumya na
kukemea kwa nguvu zote maswala haya ya ukatili wa kijinsia ili kuweza kupunguza tatizo hili.
Aliendelea kusema
kuwa ukatili wa kingono ikiwemo Ubakaji, Ulawiti pamoja na rushwa ya ngono vikikemewa kwa nguvu zote
itasaidia kwa kiasi Fulani kupunguza tatizo hili la Sonona ambalo linaathili kwa kiasi
kikubwa Uchumi na nguvu kazi ya Taifa.
Semina ikiendelea
Mwanaharakati wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo Bw. Msafiri Shababi Akitoa maoni yake kuhusu athari za Sonona.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Post a Comment