Ads

RC MAKONDA: "HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAEACHWA KWA KIGEZO CHA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA"


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amewahakikishia wanafunzi wote *waliofaulu mtihani wa Darasa la Saba* watapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza na *hakuna mwanafunzi atakaekosa nafasi kwa kigezo cha uhaba wa madarasa.

*RC Makonda* amesema kuwa *amelazimika kusitisha likizo za sikukuu* kwa watu wanaohusika na ujenzi wa *miundombini ya shule* ili kutumia muda huo kujenga na kukarabati *vyumba vya madarasa zaidi ya 431.*

Itakumbukwa kuwa *Mkoa wa Dar es salaam umekuwa kinara* wa ufaulu kitaifa kwenye *matokeo ya mtihani wa darasa la Saba* kwa kufaulisha wanafunzi zaidi ya *wanafunzi 64,861* ambapo kati ya hao *wanafunzi 31,066* ilikuwa wakose nafasi za kujiunga na *kidato cha kwanza* kutokana na *uhaba wa vyumba 431* vya madarasa jambo ambalo *RC Makonda* ameahidi *kulivalia njuga.*

*DAR ES SALAAM TUNASEMA HAACHWI MTU*.

No comments