NAIBU MEYA MANISPAA YA ILALA AWAKUMBUKA YATIMA.
Mwamba wa habari
Kuelekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ,Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbila moto ,ametoa msadaa wa vituvyakula ikiwemo mikate 100,na sukari kilo 50 kwaajili ya kuwa saidia watoto katika kituocha kulelea wato yatima cha Mwana kilichopo Vingunguti Manispaa ya Ilala.
Akizungumza wakati wa kutoa msaa huo kumbilamoto , amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli , kwa kutoa Elimu bure kwa watoto wa Tanzania ambayo imesaidia hata Watoto yatimamkusoma sawa na wengine.
“ Kwanza nishukuru kwwa kupata nafasi hii nimekuja hapa katika kituo cha Mwana cha kulelea watoto yatima nia na madhumuni ni kutoa hizi zawadi na kuwapa sikukuu ya chritmas watoto hawa”alisema
Kabla ya serikali ya awamu ya tano kutangaza na kuanza kutoa Elimu bure msingi na Sekondari watoto yatima walikosa haki ya kupata elimu kwakuwa hawakumudu kulipa lakini sasa wanapata elimu bila shida nijambo la kupongezwa na na amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kukitambua kituo hiki na pia amemshukuru Balozi wa Uturuki kwa ufadhili wa kituo hicho.
Aidha ameitaka jamii kuto kwepa majukumu ya ulezi bali ndugu , jamaa na wanafamilia wachukue jukumu la kulea watoto yatima walio potelewa na wazazi wao.
“Usia wangu kwa wazazi tuendelee kuwa lea Watoto siyo vizuri kuwaacha na kuwapeleka katika kituo cha kulea watoto ili hali munao uwezo wa kuwa saidia, Tuna ushaidi wapo watoto walitelekezwa na wazazi wao lakini baada ya kuwaona wamepata mafanikio walianza kuwakimbilia na wanajisuta nafsi zao “alisema .
Kwaupande wake Meneja wa kituo hicho Elizabeth Mwankemwa , Akizungumza Mara Baada Ya Kupokea Vyakula hivyo Amemshukuru Naibbu Meya Omary kumbilamoto kwa moyo wake wakujitoa kwa watoto hao na Kuitaka Jamii Kujitolea Kwa hali na Mali Katika Kuwansaidia Watoto hao.
“Tumefurahi sana kwa ujio wenu hapa kwa kuwashika watoto, kwaniaba ya watoto naomba Mungu awabariki sana ,mmeacha kazi zenu na kuja hapa Mungu awazidishie pale ambapo mmetoa ,na kwakweli Naibu Meya hapa si mara ya kwanza kuja kuwa saidia woto huwa anakuja mara kwa mara anauliza wana shida gani anawasaidia kwa mahitaji mbalimbali na pia anazunguza nao”alisema.
Pamoja na hayo Mkemwa ameitaka jamii kuwatembelea watoto hao hata kama hawana cha kuwapa na bali hata ile kuona watoto hao kuwa wanawatembelea wanafarijika na kujisikia kupendwa .
“Nawakarisha wanachi wote kutembelea kituo hiki si lazima uwe na fedha ama vitu hata ukija tu wewe Mama ukazunguza na watoto wa kike kuhusu malezi wanapitia mabadiliko hata akina Baba pia tuna wahitaji sana hatu hitaji ngu kuwanyoosha bali tutumie maneno sisi wametuzoea lakini akija mtu mwingine itasaidia watamsikiliza “alisema
Kituo hicho kina watoto 52 wasichana 21 wavulana 31 na wametoka maeneo mbalimbali ,kwa mujibu wa Meneja huyo kituo hicho kina kabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ,Mavazi ,Chakula ,Madafutali na miundombinu ya Mji taka huwa yanajaa marakwa mara .
Post a Comment