BAVICHA Waandika barua nzito kwa Jaji Mkuu
Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Patrick Ole Sosopi, jana Desemba 12, 2018 wamewasilisha barua katika Ofisi ya Jaji Mkuu, Ibrahim Hamis Juma jijini Dar es salaam, wakilalamikia kukiukwa kwa haki kwenye mahakama.
Patrick
Ole Sosopi amesema wamefikia uamzi huo kwa kuona hakuna sehemu nyingine
wanaweza kupata haki kutokana na viongozi wao wa kitaifa kukosa badhi
ya haki ikiwemo kuwaeleza wananchi maendeleo ya kesi zao mahakamani.
''Tumechukua
hatua ya kumwandikia barua Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, kumweleza
malalamiko yetu juu ya uonevu wanaofanyiwa viongozi wetu na vyombo vya
dola na sasa vimefika mpaka mahakamani sasa ambapo viongozi wetu wana
kesi mbalimbali lakini hawapati haki zao'', amesema Sosopi.
Aidha
Ole Sosopi, ameongeza kuwa kuna mambo mengi yanayofanyika ambayo
yanaenda kinyume na haki katika Mahakama ikiwemo kukamatwa na kupigwa
kwa wanachama wa CHADEMA wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kichama.
Pia
amesisitiza kuwa barua hiyo haiishii kwa Jaji Mkuu pekee bali inakwenda
pia kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali Dkt. Adelardus Kilangi pamoja na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Post a Comment