Wabunge wa Upinzani wasusa kuapishwa wabunge wa CCM.
Wabunge wa Chadema na wa CUF upande wa
katibu mkuu Maalim Seif wamesusia kushuhudia kiapo cha wabunge wanne wa
CCM wakati wabunge hao walipokuwa wanaapishwa.
Mkutano wa Bunge umeanza leo asubuhi Jumanne Novemba 6, 2018 na kuongozwa na Spika Job Ndugai.
Mara baada ya kumaliza dua na wimbo wa Taifa, uliwadia
wasaa wa kiapo kwa wabunge wanne waliokuwa upinzani ambao walijiuzulu na
kuhamia CCM ambako waliibuka washindi.
Wakati wa shughuli hiyo ya kiapo, wabunge hao wa Chadema na CUF upande wa Maalim Seif hawakuwapo bungeni.
Aliyekuwa wa kwanza kuapishwa ni Julius Kalanga (Monduli),
akafuatia Mwita Waitara (Ukonga), akaja Timotheo Mzava (Korogwe
vijijini) aliyepita bila kupingwa akichukua nafasi ya marehemu Stephen
Ngonyani ‘Majimarefu’ aliyefariki dunia.
Wa mwisho kuapishwa alikuwa Zuberi Kuchauka (Liwale) ambaye
awali alikuwa mbunge kupitia CUF. Mara baada ya kumaliza kuapishwa,
wabunge hao wa Chadema na CUF walirejea bungeni.
Post a Comment