SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI
Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akikagua madaftari ya
wagonjwa waliolazwa wodi ya akina mama kwenye hospitali ya Wilaya ya
Manyoni,kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.Rahabu Solomon
NA WAMJW-MANYONI
Serikali
imetangaza neema ya kupeleka gari ya wagonjwa (Ambulance) katika
Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ili kutatua tatizo linaloikabidi Wilaya
hiyo hususan ya vifo vitokanavyo na uzazi.
Ahadi
hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipoitembelea
hospitali hiyo kwa lengo la kutazama utoaji wa huduma za afya ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa Singida.
Dkt.
Ndugulile amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza kero kutoka kwa
wananchi wanaotumia hospitali hiyo ambapo wengi walisema kungekuwepo na
gari ya wagonjwa kungeepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto
pamoja na wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura.
"Naomba
niwaahidi wananchi wa Manyoni, Serikali imeagiza magari ya kubebea
wagonjwa ambayk yanaweza kufika mwezi Disemba mwaka huu,hivyo
nitahakikisha katika mgao wa magari hayo basi na hospitali hii ya
Wilaya inapata gari moja kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa
hapa. Alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Dkt.Ndugulile aliahidi kuwatafutia wataalam wa Afya watakaoweza kwenda
kupunguza uhaba wa watumishi wanaokabiliana nayo hospitali hiyo
Naye
Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Atupele Mohamed alisema
hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majengo ikiwemo chumba
cha huduma za uzazi ambapo uwezo wake kwa mwezi ni kuzalisha akina mama
90 lakini kwa sasa huzalisha wastani wa akina mama 400.
Aidha,
Dkt. Atupele alisema Hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa watumishi
wenye sifa, ambapo ina jumla ya watumishi 107 sawa na asilimia 53 ya
watumishi wanaohitajika.
Dkt. Atupele alitaja
uhaba mkubwa wa watumishi hao ni Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa
mionzi na wataalamu wa kutoa huduma za usingizi.
Katika
Wilaya hiyo Naibu Waziri huyo aliweza kutembelea kutembelea kituo cha
kulea wazee na wasiojiweza cha Sukamahela pamoja na Hospitali ya rufaa
ya Mtakatifu Gasper iliyopo Itigi na kuridhika na hali ya utoaji wa
huduma za afya katika Hospitali hiyo.
Post a Comment