Ads

CCM Buguruni wajipanga kushika dola 2019/2020



Matukio mbalimbali katika mkutano Mkuu wa jumuiya ya Wazazi tawi la Buguruni Mivinjeni Dar es Salaam  pia chama hicho kilipokea wanachama wapya na kugawa kadi Picha na Heri Shaaban



Mwambawahabari
Na Heri Shaaban
JUMUIYA ya Wazazi  Tawi la Buguruni Mivinjeni imesema Chama cha Mapinduzi CCM kinatarajia kushika dola katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa Mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020

Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Wazazi Buguruni Mivinjeni Fatuma Maneno wakati wa kusoma taarifa ya utendaji kazi ya Jumuiya hiyo ya mwaka 2017 hadi 2018  katika Mkutano Mkuu uliokuwa unaelezea mafanikio hiyo  ,changamoto,mahusiano ya jumuiya na chama pamoja na Jumuiya zingine.

"Jumuiya yetu hapa Buguruni Mivinjeni inafanya kazi kwa kushirikiana na Chama pamoja na jumuiya nyingine na kwa sasa tumejipanga kuakikisha tunachukua dola kuanzia serikali ya Mtaa hadi uchaguzi Mkuu mwaka 2020 " alisema Fatuma

Fatuma alisema kwa sasa Jumuiya hiyo inashirikiana kwa pamoja na Chama katika mikakati mbalimbali ikiwemo kukuza Jumuiya na kuongeza wanachama.

Aidha alisema mwaka 2016 hadi 2017 wanachama 97 mwaka 2017 / 2018 wanachama 146 wanaume 36 wanawake 110  .

Akielezea Mafanikio alisema wamepata mafunzo elekezi ya uongozi kwa ushirikiano wa kata na Wilaya hivyo  kufanya wawe  imara  katika utekelezaji kazi za Jumuiya ya Wazazi Mivinjeni.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Mkoa Dar es Salaam Busoro Pazi ,alisema Jumuiya hiyo wanajika viongozi wanaotumikia wanyonge wafanye kazi za wananchi, wajiepushe na Kashifa wafanye kazi kwa Weledi kwa masilahi ya Chama cha Mapindunzi CCM na Jumuiya zake .

Pia Busoro aliwataka Wazazi kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kuwataka watoto na kufuata maadili mema.

Naye Kaimu Katibu wa Wazazi Wilaya ya Ilala  Ibrahimu Saidi aliwataka Wana CCM wilaya ya Ilala kuanza kupita pita mitaani kuhudumia wananchi maeneo ambayo yamechukuliwa na wapinzani.

Ibrahimu alisema uongozi upangwa na mungu wana CCM wavunje makundi kuwa wamoja na kuakikisha chama kinashika dola  wafuate kanuni na misingi ya chama.

Naye Mjumbe  wa Kamati ya Utekeleji Wazazi Wilaya ya Ilala Shamsudin Ahmed,ameitaka Jumuiya hiyo  wanachama wake wajikubali  wasiendekeze  majungu badala yake wawe wamoja washikamane .

Mwenyekiti wa Wazazi wa Wilaya ya Ilala Lucas Lutainurwa aliwataka waongeze wanachama ili kukuza Jumuiya ya Wazazi na kuacha makundi .


No comments