Ads

MSAJILI AVIFUNDA VYAMA VYA SIASA.


 Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (kulia) akimtambulisha Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed  kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi leo jijini Dar es Salaam. 
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (kulia) akimtambulisha Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed  kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa Mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed  akisisitiza jambo kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa  kufunga  mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi leo jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakichangia mada  wakati wa mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi leo jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakifuatilia mada ya jinsi ya kuandaa taarifa za fedha kwa ajili ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakati wa mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Vyama vya Siasa nchini vimetakiwa kutumia njia rafiki katika kutafuta madaraka ikiwemo kuipongeza na kuikosoa serikali kwa kutumia hoja ili kulisaidia taifa la Tanzania kuwa na maendeleo.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya Siasa wakati akifunga Semina leo jijini Dar es Salaam, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohammed Ally Ahmed, amesema kuwa ni vizuri vyama vikawa na lengo la kuelimisha jamii pamoja kuikosoa kwa ajili ya kupatikana kwa maendeleo.

Amesema kuwa wakati umefika wa kutafuta mustakabari wa taifa ili kuhakikisha vyama vya siasa vinachangia kwa asilimia kubwa upatikanaji wa maendeleo hapa nchini.

"Nivizuri tukaikosoa serikali kwa hoja jambo ambalo litasaidia kufanikisha maendeleo" amesema Ahmed.

Amesema kuwa nchi ya Tanzania wanasiasa huwa wanatofautiana kwa hoja na sio lugha za matusi au kutumia bunduki.

Ahmed amefafanua kuwa ni vizuri kuangalia njia zetu ambazo tunatumia kutafuta madaraka kwani hakuna mtu anayeweza kukaa milele katika uongozi wake.




Septemba I9 mwaka huu Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuvijengea vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze kujiendesha kama taasisi.

Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu kutoka Ofisi yaMdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji Mtungi.

Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.

Wakati huo huo Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mkandala ambaye aliwasilisha mada ya Jinsi ya Kuendesha chama kama taasisi,amesema lengo la chama cha siasa chochote ni kujiandaa kushika madaraka au kuwa wapinzani wa serikali hivyo lazima kuhakikisha vinajijenga kama taasisi inayoaminika kwa wananchi.

Naye Profesa Mkandala amesema siasa vyama vingi hapa Nchini ni matokeo ya ukoloni mamboleo ambao ulianza kushamiri hapa nchini kwa miaka 1990 ambapo nchi ya Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Barani Afrika zilikumbwa na mabadiliko ya kiuchumi ya soko huria ikiwemo nchi zilizokuwa za ujamaa kuanza kufuata m asharti ya Shirika la Fedha Duniani IMF.

Aidha Profesa Mkandala alitaja vigezo vinavyofanya chama kuwa Taasisi muhimu kuwa ni Itikadi, Uongozi bora, Wanachama, Sera na programu za chama, Rasilimali watu na Rasimali fedha pamoja na watu ambao wako tayari kujitoa kwa ajili ya chama.

Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa imeandaa mafunzo haya ya Siku mbili ili kuwajengea uwezo viongozi wa Kitaifa wa  vyama siasa kuendesha vyama vyao kama taasisi na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi ambayo yamemalizika leo.




No comments