CCM YAFUNGA KAMPENI JIMBO LA UKONGA.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Mongolandege Jimbo la Ukonga Rajab Tego wakipongezana na Mbumge wa Jimbo la Nzega Tabora Mhe. Hussein Bashe leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM Jimbo la Ukonga.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Mongolandege katika Jimbo la Ukonga Rajab Tego wakwanza kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa Chama cha CCM leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Mongolandege katika Jimbo la Ukonga Rajab Tego akiwa katika mkutano wa kufunga Kampeni za CCM katika Jimbo la Ukonga leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) Dkt. Ally Bashiru pamoja na wabunge leo wamefunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, huku wakitaka wananchi kumchagua mgombea wa Ubunge katika Jimbo hilo Mwita Waitara katika uchaguzi utakaofanyika kesho Septemba I6 mwaka huu.
Baadhi ya Wabunge wa CCM walioshiriki kufunga kampeni za Uchaguzi katika jimbo la Ukonga ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Ritta Kabati, Mbunge wa Nzega Tabora Hussein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile.
Akizungumza katika Mkutano wa kufunga Kampeni za CCM leo jijini Dar es Salaam Dkt. Bashiru, amesema kuwa wananchi wa Jimbo la Ukonga wanapaswa kuendelea kumuamini kwa kumchagua Waitara katika uchaguzi utakofanyika kesho.
Amesema kuwa Waitara ni kiongozi mchapa kazi kwani ameanza kumjua tangu akiwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
"Waitara ni kiongozi mzuri akiwa chuo alifanya vizuri kwa kuwaongoza wanafunzi wezake na bila kupinduliwa muda wote katika uongozi wake akiwa Chuo" amesema Dkt. Bashiru.
Ameeleza kuwa ni mtu makini katika utendaji wake na bila shaka ataendelea kulitumikia taifa la Tanzania katika Jimbo la ukonga.
Amesema kuwa CCM itaendelea kutekeleza Ilani yake kwa vitendo ili kuhakikisha inaleta maendeleo na kuaminika kwa watanzania wote.
"Kuna miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali ya CCM ambayo itasaidia kuinua uchumi wa Tanzania" amesema Dk. Bashiru.
Katika hatua nyengine Dkt. Bashiru amesema kuwa ndani ya CCM kulikuwa na baadhi ya watu wanatumia fedha zao kupata cheo, lakini kwa sasa uwezo wa mtu ndio anapewa kipaombele katika nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama.
"Tunataka kujenga Chama ambacho kinajitegema kifedha na sio kutegemea wafadhili ambao wamekuwa wakila rushwa"amesema Dkt. Bashiru.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, amesema kuwa katika uchaguzi utakofanyika kesho amejipanga kuimarisha ulinzi kila mahali ili kuhakikisha wapiga kula wanamchagua kiongozi wanampenda katika hali ya amani.
Mhe. Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa ulinzi Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kupiga kula bila kuwa na hofu yoyote katika uchaguzi.
"Tumejipanga kuweka ulinzi hivyo msiwe na shaka wala hofu, naomba mjitokeze katika vituo vya kupiga kula" amesema Mhe. Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, amesema kuwa wilaya yake imejipanga kila idara ili kuhakikisha amani inatawala katika uchaguzi huo utakaofanyika kesho.
"Tumejipanga kuhakikisha ulinzi unakuwa katika maeneo yote, wapigakula baada ya kupiga ludini nyumani kazi ya kulinda kula wachieni mawakala" amesema Sophia Mjema.
Kwa upande wake Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, amewatakaa wananchi wa jimbo hilo kumchangua tena ili kuendelea kuwaletea maendeleo.
Waitara amesema kuwa ameamua kiludi CCM kutokana na utendaji wa Rais Dkt. Magufuli kwani anaamini maendeleo yataendelea kupatika akiwa ndani ya CCM kila kitu kitakwenda sawa katika Jimbo la ukonga.
Post a Comment