DR MENGI ATOA SABABU YA KUANDIKA KITABU
Dkt,
Reginald Mengi amebainisha hayo leo Julai 02, 2018 wakati alipokuwa
anazungumza mbele ya wageni viongozi wa nchi na wageni waliohudhuria
katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chake kilichopewa jina la 'I Can, I
Must, I Will- The Spirit of Success' iliyofanyikia katika ukumbi wa
Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.
"Nilikuwa
na mtoto Roodney lakini kabla hajaondoka hapa duniani aliniomba sana
niandike kitabu ambacho kitacho kuwa kinaelezea maisha yangu na mambo
ambayo nimeyafanya kwa hiyo nimefanya hivyo kama alivyotaka mwanangu na
leo namshukuru Mungu nimeweza kutimiza ahadi yangu", amesema Dkt.
Mengi.
Pamoja
na hayo, Dkt. Mengi ameendelea kwa kusema "ahadi ya pili aliyonipa ni
kunitaka niwe naenda kufanya mazoezi kila siku 'gym' lakini huwa nafanya
hivyo mara tatu au nne nasio kila siku, ila kuanzia leo nitamiza hilo".
Mbali
na hilo, Dkt. Mengi amesema jambo kubwa lililoweza kumsukuma mpaka leo
hii kukizundua kitabu chake hicho ni kutokana na yeye kuzaliwa katika
maisha ya kimasikini kitu ambalo ametaka wananchi wafahamu hilo ili nao
waweze kujua namna ya kutoka huko na kuwa katika maisha mengine.
Kwa
upande wake, Rais Dkt. John Magufuli ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi wa
hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha 'I Can, I Must, I Will- The Spirit
of Success' amewataka watanzania na wafanyabiashara wote kiujumla
kununua kitabu hicho ili kiweze kuwafundisha katika kutokana na hali ya
umasikini huku akiwasisitizia zaidi kufanya kazi kwa bidii na kuacha
kusikiliza maneno ya watu ambao wanawakatisha tamaa.
Post a Comment