Wizara yazindua mradi wa VVU na Ukimwi kwa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Nchini
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba
akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya
VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida.
Naibu Meya wa Manispaa ya Singida Mhe.Yagi Kiaratu akitoa
neno la shukrani kwa viongozi wa Wizara hawako pichani wakati wa uzinduzi wa
mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake
vijana leo Mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Margaret Mussai akiongea na
wajumbe wa Mkutano hawako pichani wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia
maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani
Singida.
Uongozi
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida,
Taasisi za TASAF na TACAIDS na wadau wa maendeleo kutoka Amref na TAYOA
wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wa
uzinduzi wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na
wanawake vijana leo Mkoani Singida.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano
WAMJW
Na Anthony Ishengoma Singida.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU na
Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana leo Mkoani Singida kwa lengo la
kuutambulisha kwa jamii kuhusu wasichana na wanawake vijana walio shuleni na
walio nje mfumo wa Elimu.
Mradi huu unatekelezwa na Wizara pamoja na wadau wa Maendeleo kutoka
AMREF, TAYOA, TASAF, TACAIDS na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund na wakati huu
mradi uko katika hatua ya majaribio katika mikoa mitatu ya Tanzania ambayo ni
Singida, Dodoma na Morogoro.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa
mradi huu mapema leo mjini Singida Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Marcel Katemba amesema kimsingi Wizara
yake imepewa jukumu la kuandaa mazingira rafiki na wezeshi ya utekelezaji wa
Mradi huu na ndiyo maana hatua ya awali ya maandalizi inaanzia kwa kujenga
uwezo kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka mikoa ya majaribio ya mradi.
Aidha Bw. Katemba amesema
Serikali ya Tanzania imepata ruzuku kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund
kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi Nchini kwa kipindi cha January 2018 mpaka Desemba
2020.
‘’Maambukizi ya Ukimwi pamoja na
mambo mengine yanachangiwa na tabia za Wasichana balehe na Wanawake vijana
wenye umri wa miaka 10-24 kwa kujaribu kufanya mambo yanayotokana na mabadiliko
ya miemko ya miili yao ambayo yanasababisha kujamiina na mahusiano ya kimapenzi
yasiyokuwa salama.’’Alisema Kaimu Katibu Mkuu Marcel Katemba.
Aidha ameongeza kuwa mradi huu wa
VVU na Ukimwi kwa wasichana balehe na Wanawake Vijana ambao utatekelezwa kwa
Halmashauri 10 kutoka mikoa mitatu ya majaribio ambayo ni Manispaa ya Singida,
Iramba, Halmashauri ya Singida, Dodoma, Bahi, Mpwapwa,Kongwa na Kondoa na kwa
mkoa wa Morogoro mradi huu utaendelea kwa Halmashauri za Ulanga, Malinyi na
Ifakara.
Wakati huo huo Naibu Meya wa Mkoa
wa Singida Bi. Yagi Kiaratu amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Mkoa
Singida bado ni Changamoto kubwa na kusema kuwa ujio wa mradi huu mkoani kwake
utachangia kupunguza kuenea kwa virusi hivyo kwa wasichana balehe na wanawake
vijana kwa kupunguza au kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
Bi. Yagi ameongeza kuwa tatizo
kwa wasichana wengi walio katika rika hili wanaingia katika janga la ukimwi
kwasababu bado wanakuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu janga hili lakini pia
wanakuwa hawajaanza kujitambua kama wako katika hatari ya kupata maambukizi ya
ukimwi.
Jitihada za kupambana na ugonjwa
wa Ukimwi zimekuwa zikiendelea kwa kipindi cha miongo mitano lakini kwa kuwa
tatizo hili changamoto kwa maendeleo ya Familia na Taifa serikali inaendelea
kuokoa maisha ya watu hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakuu.
Post a Comment