WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MADINI NA KUZINDUA MAABARA YA KISASA YA MADINI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi wananchama wa Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye Kituo cha Utafiti na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kundichi jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Meneja wa Maabara ya Kemia na Mazingira wa Kituo cha Utafiti na Uendelezaji wa Sekta ya Madini, Bw. Charles Butete baada ya kuzindua maabara hiyo , kunduchi jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya kufungua Mkutano 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi hizo kwenye Kituo cha utafiti na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kunduchi jijini Dar es salam, Juni 8, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mkutano wa 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye Kituo cha utafiti na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kunduchi jijini Dar es salam, Juni 8, 2018.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
……………..
*Ni ya kwanza Afrika, inauwezo wa kutambua aina za madini na yalikotoka
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya na ya kwanza barani Afrika yenye uwezo wa kupima na kutambua aina mbalimbali za madini.
Amesema maabara hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya umiliki wa madini na kudhibiti utoroshwaji wa madini mbalimbali kati ya nchi moja na nyingine.
Maabara hiyo imefunguliwa leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) katika Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC) kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema uzinduzi wa maabara hiyo utawezesha wataalamu kutambua aina za madini na nchi yanakotoka, hivyo kuondoa migogoro ya umiliki wake.
“Maabara hii litatuweza kulinda madini yetu na kufanya biashara ya madini vizuri. Pia hii ni fursa nzuri kwa nchi za Afrika kutumia maabara hii kupima madini yao na kubaini yalikotoka,” amesema.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha wanaziwesha nchi wanachama kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya madini pindi zinapohitaji.
Pia Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara hiyo pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu watakaoiendesha.
Waziri Mkuu, pia ameiomba Serikali hiyo kutoa mafunzo hayo kwa Watanzania wengi zaidi ili kuongeza idadi ya wataalamu wa kuendesha maabara hiyo.
Pia, Waziri Mkuu amefungua Mkutano 38 wa Mawaziri wa Madini kutoka nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika katika kituo cha AMGC.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama zilizosheheni wanyama wa aina mbalimbali pamoja na fukwe za bahari
Post a Comment