Ads

DC MJEMA AWATAKA WATANZANIA KUWA NA UTAMADUNI WA KUSAFISHA MAZINGIRA.

Mwamba wa habari
Na. John Luhende 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amewataka wananchi Wilayani Ilala  kuwa na utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo korofi.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya siku ya mazingira katika Manispaa ya Ilala, Mhe. Mjema amesema kuwa ni vyema kutuza mazingira yetu ili kuhakikisha tunaishi katika sehemu rafiki.

"Leo katika wilaya ya ilala tunafanya maadhimisho ya siku ya mazingira kwa kufanya usafi katika fukwe za bahari, ni vizuri kuendelea ili mazingira yetu yawe safi muda wote" amesema Mhe. Mjema.

Amesema kuwa katika wiki hii ya usafi kesho wataendelea kufanya usafi maeneo ya Zakhiemu Mbagara.

"Imefika wakati kila mtu anapaswa kuwajibika kwa kuhakikisha anachangia fedha yaa utoaji taka jambo ambalo linaweza  kutatua changamoto ya uchafuzi wa mazingira" amesema Mapunda.

Mapunda ameeleza kuwa Manispaa itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utuzaji wa mazingira ili kuhakikisha kila maeneo yanakuwa safi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni uzoaji taka ya Green Waste Pro Ltd Anthony Shayo, amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo ni ukosefu wa elimu juu ya utuzaji wa mazingira.

Shayo amesema kuwa wananchi wanapaswa kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa kutuza mazingira pamoja na kuwa na utamaduni wa kujitolea katika kufanya usafi maeneo mbalimbali ambayo yameonekana korofi.
Katika hatua nyengine, Mhe Mjema amemtaka mkuu wa kituo cha polisi cha Surrender bridge kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdon  Mapunda, amesema kuwa Manispaa  ya ilala wamekuwa na utamaduni wa kufanya usafi katika fukwe za bahari.

Ameeleza kuwa licha ya kuendelea kufanya usafi, siku ya leo wamefanya  uzinduzi wa maadhimisho ya mazingira na kufanya usafi katika fukwe ya ocean road ili kendelea kutoa elimu kwa watanzania.













No comments