DKT TIZEBA- WAKULIMA 11,177 WA UFUTA WANUFAIKA NA MRADI WA FARM AFRIKA
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Farm Afrika Ndg Ryan Whalen akizungumza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
Baadhi ya wadu waliohudhuria mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.
Na Mathias Canal-WK,
Dar es salaam
Mwamba wa habari
Utekelezaji wa mradi wa
Farm Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu umeweza kuwafikia wakulima takribani
11,177 ambapo kati yao wanawake ni 5,474 na wanaume ni 5,703 huku kati ya wakulima
hao vijana wakiwa ni takribani 5,821 yaani zaidi ya nusu (52%) kutoka wilaya ya
Bahi, Manyoni na Babati.
Hayo yamebainishwa juzi
22 Juni 2018 na Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza
kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya
uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli
Jijini Dar es salaam.
Dkt Tizeba alipongeza
jitihada hizo kwani zinachangia kukuza kipato cha wakulima na uchumi wa nchi kwa
kuingiza fedha za kigeni huku akiwataka watumishi mbalimbali kuwaunganisha
wakulima wadogo wadogo katika masoko rasmi na kujenga uelewa wao juu ya
vichocheo na fursa za ushiriki endelevu.
Waziri huyo wa kilimo
alilishukuru shirika la Farm Afrika kwa kuona umuhimu na fursa zilizopo katika
kilimo cha ufuta katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara hivyo kuwanufaisha
wakulima kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa katika zao hilo.
Alisisitiza kuwa zao la
ufuta lina fursa kubwa ya soko ambapo kwa sasa mahitaji ya soko ni zaidi ya mara
tatu ya kiasi kinachozalishwa kwa mwaka ambapo hali hiyo inatokana na nafasi
kubwa kwa wakulima wa ufuta kujipatia kipato na kuboresha maisha yao.
Alisema kuwa serikali
inaweka mkazo mkubwa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta na
juhudi hizo zinajidhihirisha katika hatua ambazo serikali inaendelea kuzichukua
kwa kuhakikisha uzalishaji wa mbegu za mafuta ndani ya nchi unaongezeka.
Alisema, kupitia
utekelezaji wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili mbegu za
mafuta ikiwa ni pamoja na ufuta na alizeti ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele
ambapo kwa kuanzia msimu wa mavuno ujao zao la ufuta litaingizwa kwenye mfumo
wa stakabadhi za ghala na katika kuimarisha upatikanaji wa soko la ziada kwa
zao la ufuta na mbegu nyingine za mafuta, Na kuongeza kuwa Bodi ya mazao
mchanganyiko kuanza kununua mazao hayo ili kuhakikisha mkulima anapata soko la
uhakika zaidi.
Katika hatua nyingine,
Mhe Dkt Tizeba aliwasihi wakulima wa ufuta kote nchini kubadilika kuanza kufanya
kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea cha kujikimu ikiwa ni pamoja
na kujua mahitaji ya soko kwa maana ya ubora wa ufuta na kiasi, kutumia
teknolojia hususani zana bora, mbegu bora na mbolea sambamba na kujiunga katika
vikundi au ushirika na kuuza kwa pamoja na kuwa na nguvu ya pamoja.
Post a Comment