DC MJEMA AFUTRISHA WATOTO YATMA ,ATOA NENNO KWA VIONGOZI WA DINI
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Viongozi wa
dini Wilayani Ilala wametakiwa kusaidia katika kufundisha maadilimema kwa
watoto ili wabaki na maadili na tamaduni za kitanzania ,na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi
hao.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati akitoa neno lashukra katika
Futari aliyo waandalia Watoto yatima wa
wilaya hiyo ambapo pia vingozi wa dini mbalimbali na wanachi walijumuika pamoja .
‘’Viongozi
wetu wa dini tuna taka tuwatumie kunapokuwa na mambo magumu tutaendelea
kushirikiana nayi katika yote tunayo fanya masuala ya imani yanahitajika
naninyi ndiyo kazi yenu ushirikiano huu hautaishia kwenye Futari,’’alisema
Aidha
amewataka wananchi kuitunza amani yanchi
na kuwataka kufanya kazi kwa bidii kuijenga nchi na ikiwa kunajamba ambalo
haliendi sawa wasisite kutoa ushauri kwa vongozi wao ili kuendeleza amani na
umoja wa kitaifa .
‘’ kila
mmoja wetu afanye kazi na awe mmbunifu ili kuendeleza Tanzania ya viwanda na
kwa mlio kuwa mmefunga tueendelee kuwa wasafi tusije kuhabu tena kwa
siku zilizobakia,’’ alisema
Pamoja na
hayo Mhe. Mjema amewashukuru madiwani wa
Maispaa ya Ilala kwa umoja wao bila kujali itikadi zao za kisiasa na
kushirikiana kwa kila jambo na kufanikisha mabo mbalimbali ya maendeleo bila
ubaguzi na kuwataka kuendelea na moyo
huo huo kwa sikuzijazo.
Kwaupande
wake Shekhe wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu amewataka waislam kuzingatia
maagizo ya viongozi wao katika kuswali swala ya Eid itakayo swaliwa kitaifa
katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Post a Comment