WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA – WAZIRI MKUU
Hussein Ndubikile
Mwambawahabari
Serikali imesema Jiji la Dar es Salaam kila mwaka hutumia tani 500,000 za mkaa huku ikibainisha hekta 372,000 za miti hukatwa kwa matumizi ya mkaa hali inayohatarisha mazingira ya nchi.
Aidha imewataka wananchi kuachana na matumizi ya mkaa badala wajikite katika matumizi ya nishati mbadala ili kuepukana na uharibifu wa mazingira.
Hayo yamesemwa leo jijini humo na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayoaddhimishwa kitaifa mkoani hapa huku kilele chake kitaadhimishwa Juni 5 mwaka huu.
Amesema ripoti ya mazingira ya mwaka 2014 imebainisha kuwa asilimia kuwa ya mkaa inatumika kwenye miji mikubwa inayotumia nishati ya mkaa na kwamba kiwango hicho kinahatarisha ustawi wa mazingira ya nchi.
“ Lengo la kuadhimisha siku hii kuikumbusha jamii kuweka mazingira katika hali nzuri kwa kuyatunza mazingira ili yawatunze,” amsesema.
Amebainisha kuwa kauli mbiu ya kidunia ya maadhimisho ya siku hiyo unasema dhibiti uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na plastiki huku akiongeza kuwa katika Msitu wa Kazimzumbwi kuna uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na uvamizi.
Amefafanua kuwa wiki ya maadhimisho hayo itakuwa na matuukio mbalimbali ikiwemo mijadala na makongamano na kwamba siku ya kilele zawadi zitatolewa kwa wadau walioshiriki vyema kuyatunza mazingira.
Amezisisitiza taasisi za umma na binafsi kuachana na matumizi ya mkaa na kuzitaka kuanza kutumia nishati mbadala lengo likiwa kupunguza ukataji miti.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba amesema asilimia 70 ya mkaa wote unatumika katika jiji la Dar es Salaam licha ya kuja gesi kutoka mkoani Mtwara.
Makamba amesema asilmia 61 ya mikoa zaidi ya kumi ni nusu jangwa kutokana na ukataji miti na kwamba ekari milioni nane za miti zinakatwa kila mwaka.
Naye Kaimu Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam,Mhandisi Evarist Ndikilo amesema takwimu za mwaka jana zinaonyesha hekta 46,942 zinateketezwa na mkaa huku asilimia 70 ya mkaa ukitoka mkoa wa Pwani.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Khamis Kigwangallah amesema tayari juhudi za dhati zimeshafanyika kukabiliana na uvamiizi katika msitu huo.
Post a Comment