WAZIRIMKUU MAJALIWA AGAWA ZAWADI KWA WASHINDI WA KUHIFADHI QURAN TUKUFU ASISITIZA AMANI.
Mshindi wa Juzuu 30 ni Mbwana Dadi Abdalah kutoka pemba kaskazini Zanzibar katika Taasisi ya AL-HIKIMA ambaye amepata zawadi ya shilingi milion 15.
Mwambawahabari
Na. John Luhende
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Amezitaka taasisi za dini kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza elimu nchini.
Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya kuhifadhi kura I yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yaliyo andaliwa na taasisi ya AL-HIKIMA FOUNDATION, ambapo ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani iliyopo nchi.
"Amesema tofauti za kidini hazikuanza leo bali zilikuwepo tangu zamani hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu likapewa nafasi na dini zote" Amesema.
Mashindano hayo mwaka kesho mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
"Wakati niko hapa mbele nimepokea simu kutoka kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli akaniuliza hao wote walio jana uwanja ni Waislam? nikamwambia ndiyo, akauli za tena nawewe ni mgenirasmi miaka miwili mfululizo? Nika sema ndiyo, akasema mwakani mimi nitakuwa mgeni rasmi na huyo shekh wa msikiti wa Maka nitamleta nitakuwa naye hapo" alisema Majaliwa.
Pamoja na hayo Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi zawadi kwa Washindi wa mashindano hayo.
Mshindi wa juzuu tatu kutoka AL-HIKIMA Salah, Yasir juma amepata zawadi ya 800,000
Mshindi wa juzuu tano kijana kutoka madrasa ya alhkima Mohamed. Ahmed zawadi milioni 1.
Mshindi juzuu kumi Bilal Saleh Abdalah zawadi milioni 1.2
Mshindi Juzuu 20 kutoka Bakari Athumani kutoka Mbagala zawadi milioni 1.5
Mshindi wa Juzuu 30 ni Mbwana Dadi Abdalah kutoka pemba kaskazini Zanzibar katika Taasisi ya AL-HIKIMA zawadi milion 15
Baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Waziri wa Dini kutoka Saudia Arabian, Dr Saleh bin Mohamad bin Abdullah Azizi Alshekh.
Post a Comment