Wajasiria mali wanawke Kisarawe watakiwa kuanzisha mtandao
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM), Zainab Vullu, amewataka wanawake wajasiriamali Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, kuanzisha mtandao maalumu wa kibiashara utakaowawezesha kutengeneza na kuuza bidhaa zao ili kuhimili soko.
Pia, amewahimiza kutumia mikopo wanayopata kwa tija kwa kuelekeza kwenye shughuli za ujasiriamali zinazo weza kuwaingizia kipato badala ya kuendekeza kununua mavazi na kutunzana katika sherehe .
Ameyasema hayo, jana, alipokuwa akizindua mafunzo ya wajasiriamali wanake wilayani humo, yanayoendeshwa na Kampuni ya East Africa General Business katika mkoa wote wa Pwani.
Mbunge huyo, alisema, mafunzo hayo ni lazima yawawezeshe wanawake wajasiriamali wa wilaya ya Kisarawe kuunda mtandao mmoja imara ambao utawasaidia kuwaleta pamoja na kuuza, kuuza bidhaa zao na kuwafikia wateja.
“Mtandao huu utawezesha pia kutambua aina ya bidhaa mnazo takiwa kutengeza. Kama mwenzio anateneza aina Fulani ya bidhaa siyo lazima na wewe utengeneze hiyohiyo.Tafuta bidhaa nyingine bora zaidi itakayokupatia wateja wengi,”alisema Vullu.
Aliongeza; “Kuhusu mikopo hii ndiyo inayowakwamua wanawake tatizo ni riba kubwa inayotozwa ambapo wengi wenu mnashindwa kurejesha na kukuta mali zenu zinauzwa,”
Alisema, elimu mnayopata katika mafunzo hayo iwe ni njia bora ya kuwavusha kwa kutambua matumizi bora ya mikopo na kuirejesha kwa wakati ili mikopo hiyo iwainue kiuchumi.
“Msishindane kuvaa au kutuza fedha katika sherehe.Rejesheni mikopo kwa wakati ili iwanufaishe wengine,”alisema Mbunge huyo.
Aliwataka wanawake hao wajasiriamali wilayani humo kutokuoneana wivu usio na tija, bali wivu wa kimaendeleo hususan kutengeneza bidhaa bora zinazoweza kuhimili ushindani katika soko.Kuweni wabunifu,”alisema.
Alionya wajasiriamali hao kuepuka propaganda za kisisa katika shughuli za maendeleo, kwani serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Maguli haina itikadi katika suala la maendeleo.
Alionya wanawake hao kuachana
Mkurugenzi wa kampuni inayotoa mafunzo hayo, Alexender Mallya, alisema, zaidi ya wanawake 100 wanapata mafunzo hayo wilayani humo ambapo mafunzo yataenda katika wilaya zoteza mkoa wa Pwani.
“Mafunzo yanalenga kumpatra mwanamke wa Kisarawe elimu ya kiuchumi itakayomwezesha kumpatia mbinu ili aweze kuendana na sera ya swerikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ya ya kulifikisha taifa katika uchumi wa kati,”alisema Mallya.
Pia kupata masoko ya uhakika kwa aajili ya bidhaa zao kwani changamoto kubwa inayowakabili wajasiriamali wengi ni soko la uhakika.
“Wataunganishwa na fursa za rasilimali ingawa mtaji ni uwezo wao wa kubuni wazo la shughuli ya kujiingizia kipato.
Afisa Maendeleo ya Jamii, wa Wilaya ya Kisarawe, WAnchoke Chinchibera, aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa mafunzo hayo wilayani humo ambapo alisema anaamini yatamuinua mwanamke , jamii na hata taifa zima.
Post a Comment