MASHINDANO YA UMITASHUMITA WILAYA YA ILALA YAANZA RASMI, NIDHAMU NA KUJITUMA VYASISITIZWA.
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mashindano ya michezo kwa shule za msingi UMITASHUMITA katika Manispaa ya Ilala leo yanezinduliwa rasmi ambapo michezo ya ainambalimbaliitachezwa ili kupata wawakilishi wa Wilaya.
Akizungumza na hadhara katika ufunguzi wa michuano hiyo inayofanyika katika viwanja wa chuo cha Magereza Ukonga, Kaimu Kamishina wa Magereza Gideon Nkana , ameipongeza timu za michezo zitakazoshiriki katika m chuo wa kupata timu ya Wilaya itakayowakilusha katika mashindano hayo kwa ngazi ya Mkoa na kuwataka wanamichezo kuwa na nidhamu na kujibidisha ili waweze kutetea Ubingwa wao.
Aidha amesema, Taifa bila Michezo hali wezi kujipambanua nakuharakisha maendeleo kuelimu, kiuchumi, kijamii na Kiutamaduni hivyo pamoja na changamoto zilizopo michezo mashulleni hainabudi kuendelezwa na changamoto hizo ziweze chachu ya kuendeleza michezo.
"Hapa tunaondoka Kuna KLASTA nne nawaomba ni mchezo kwa nidhamu ya hali ya juu hapa ndipo mnatakiwa muonyeshe vipaji vyenu michezo ni ajira hapa ndipo m naweza kuendeleza vipaji vyenu na serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto" . Alisema.
Amesema sekta ya Michezo inakabiliwa na changamoto ikiwemo ukosefu wa Viwanja vya michezo na rasilimali fedha lakini Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuzungumza na kuboresha baadhi ya mambo.
"Napenda niwajushe kuwa nimekubali kuwa mlezi wenu na Nina ahidi kushirikiana na viongozi wenu nanitawapa ushirikiano wa kutosha." Alisema.
Kwa upande wake Afisa Elimu msingi wa Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas, amesema mashindano hayo yameandaliwa katika hatua ya mchujo na wamegawa katika KLASTA nne katika wilaya ili kurahisisha kuwapata washindi watakao wakilisha Wilaya katika mashindano ya Mkoa.
Hongera sana Malkia wa nguvu Mama Thomas kwa uongozi wako.
ReplyDeleteMungu akuangazie zaidi katika utendaji kazi wako.
Hakika wewe ni kiongozi.