Ads

DC MJEMA:LENGO LETU NI KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI KUUZA BIDHAA ZAO NA KUJITANGAZA ZAIDI


Image result for picha za sophia mjema

Na Mussa.N.khalid
Wadau wa ujasiriamali wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wametakiwa kuendelea kuonyesha ubunifu katika utengenezaji wa bidhaa zao ili ziweze kuwa na tija kimataifa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya wajasiriamali yaliyoanza mei 15 na kuhitimishwa hii leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini hapa.

Mkuu wa wilaya Mjema amesema serikali ya wilaya ya Ilala lengo lake ni kuhakikisha wanaonyesha jitihada za kuwasaidia wajasiriamali kuweza kujitangaza zaid ili bidhaa zao zitoke mpaka nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga Stephen Lusinde pamoja na Mjasiriamli Neema Manase wamesema wanaendelea kufanya shughuli zao za utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili kuiunga mkono seriukali.

No comments