BENKI YA TPB Pls YAWEKA REKODI KIUTENDAJI,SASA MTAJI WAKE WAFIKIA SHILINGI BILIONI 60
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Pls Sabasaba Moshingi (kushoto) akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa shukrani kwa Serikali kutokana na uamuzi wa kuinganisha benki hiyo na Benki ya Twiga Bancorp.Kulia ni Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa Benki ya TPB Jema Msuya
..........................................................................................................................................................................
*Ofisa Mtendaji Moshingi aipongeza Serikali kwa uamuzi wa benki
hiyo kuunganishwa na Twiga Bancorp
BENKI ya TPB Pls imesema imeweka rekodi nzuri ya utendaji katika
kipindi cha miaka 6 iliyopita ambapo hadi sasa mtaji wake umeongezeka kutoka Sh.
bilioni 8 mwaka 2010 hadi kufikia zaidi ya Sh.bilioni 60.
Imefafanua aidha kwa mwaka
2017, benki ya TPB ilitoa gawio la zaidi ya Sh. bilioni moja kwa Serikali ambaye
ndiye mwenye hisa nyingi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa
benki hiyo Sabasaba Moshingi wakati anatoa shukrani zake kwa Serikali kutokana
na uamuzi wake wa kuamua kuiunganisha benki hiyo na pamoja na Benki ya Twiga
Bancorp.
Akifafanua kuhusu benki hiyo amesema katika kuendelea kutekeleza
majukumu yao benki ya TPB kwa mwaka 2017 ilipata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni
18.4 ikilinganishwa na faida ya Sh.bilioni 15.7 iliyopatikana mwaka 2016.
Amesema matokeo hayo ya awali kwa robo ya kwanza ya mwaka 2018
inaonyesha mwaka huu faida inaweza kuongezeka zaidi ya kiwango cha mwaka jana.
"Tunatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kutuamini
benki ya TPB kwa kazi tunayofanya kwa raia wa Tanzania, na tunahaidi tunaongea
ufanisi zaidi, na kuwafikia walengwa wote katika jamii yetu,"amesema.
Kuhusu benki hiyo kuunganishwa na benki ya Twiga Moshingi amesema
Mei 17 mwaka huu Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa niaba ya Serikali, imeamua
kuziunganisha benki hizo na kuunda benki madhubuti itakayojulikana kama benki
ya TPB na kusisitiza kuunganishwa kwa benki hizi mbili kunatokana na kutetereka
kwa mtaji wa benki ya Twiga.
Moshingi amesema anaishukuru Serikali kwa kuiamini benki ya TPB
pamoja na menejimenti yake, na kuamua kuziunganisha benki hizo ili kupata benki
moja yenye nguvu na kuongeza ufanisi.
Amesema kuunganishwa kwa benki hizo kunazaa benki moja imara ya
TPB Bank Plc, ambapo wafanyakazi, wateja, amana pamoja na rasilimali zote
zilizokuwa za Twiga Bancorp zitahamishwa kwenda TPB Bank Pc.
"Nachukua fursa hii kuwatoa hofu wateja wote waliokuwa na
amana zao kwenye benki ya Twiga kuwa wasiwe na hofu kwani amana zao ziko salama
kabisa, na wataendelea kupata huduma zote za kifedha kupitia kwenye matawi yao
ya Twiga kwa muda, wakati taratibu zinafanyika ili kupata huduma hizo kwenye
matawi yetu benki ya TPB mara baada ya taratibu ya kuunganishwa kwa mifumo ya
benki hizi mbili utakapo kamilika,"amefafanua.
Moshingi ameongeza kuwa hata hivyo mashine za kutolea fedha za
benki hizo mbili ziko kwenye mtandao mmoja na hivyo wateja wake wote
wataendelea kupata huduma kama kawaida.
Post a Comment