WAKULIMA WA PAMBA ZINGATIENI MAELEZO YA WATAALAMU ILI MPATE TIJA: DKT.NCHIMBI.
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka wakulima wa pamba kuachana kilimo cha mazoea bali watakiwa kuzingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu ili waweze kuwa na kilimo chenye tija ambacho kiawasaidia kuokoa mazao yao yasiendelee kushambuliwa na wadudu waharibifu.
Hatua hiyo itasaidia kuondokana mapungufu ambayo yamekuwa yakijitokeza wakati wa upuliziaji wa viua wadudu ambavyo vimekuwa vikisababisha baadhi ya pamba ya wakulima kushambuliwa na wadudu waharibifu.
Kauli hiyo jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Rehema Nchimbi wakati ukaguzi mashamba mbalimbali ili kujionea uendeshaji wa zoezi la unyunyuziaji wa viua wadudu katika mashamba ya wakulima wilayani Igunga.
Alisema mkulima ni lazima azingatie maelezo yale anayopewa na Wataalamu wa kilimo kuanzia kupanda, kupalilia, kunyunyuzia dawa na kuvuna ili aweze kupata mavuno mazuri yatakamwezesha yeye kupata maendeleo na taifa kwa ujumla.
Dkt. Nchimbi alisema Serikali imeadhimia kuhakikisha kuwa wakulima wa pamba na mazao mengine wanatumia zao hilo katika kubadilisha maisha yao na kuwa wachangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa nchini.
Aidha Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka viongozi ,watendaji kutowaacha wakulima waangaike pekee yao katika kipindi hiki cha kupambana na wadudu waharibifu katika mashamba yao bali washirikiane nao kama timu ili kuhakikisha kuwa hakuna mapungufu ambayo yatamkwamisha mkulima kufanya vizuri katika uzalishaji wake.
Dkt. Nchimbi alisema haiwezekani wasubiri hadi msimu umalizike ndio waanze kushughulikia mapungufu yaliyojitokeza bali kila wakati inabidi viongozi kwenda kwa wakulima ili kujua shida zinzowakabili katika uzalishaji wao.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuwamfanya wakulima waweze kuona kilimo cha pamba na mazao mengine kina tija kwao na kinaweza kuwakomboa katika maisha yao na kukiona kuwa kinaweza kuwatatulia matatizo yao.
Kwa upande wa Bwana Shamba kutoka Kampuni ya Olam Tanzania Limited Onesmo Daniel alisema baada ya kutembelea mashamba mbalimbali ya wakulima wamegudua kuwa kutokufa kwa wadaudu waharibifu katika zao la pamba hakutokani na ubora wa dawa bali ni baadhi ya wakulima kutofuata maelekezo ya wataalamu wakati wa unyunyuziaji viua wadudu katika zao hilo.
Alisema wapo wakulima ambao wamekuwa hawachanganyi dawa na maji vizuri na hivyo kufanya sehemu ya mimea shambani kupata dawa na mingine kupata maji tu na hivyo kufanya wadudu waharibifu kuendelea kuwepo shambani.
Daniel aliongeza kuwa tatizo jingine ni wakulima kuendelea kutumia utaratibu wa zamani wa kwenda kasi wakati wa unyunyuziaji ambao umekuwa ukisababisha baadhi ya mimea kurukwa na hivyo kuwa chanzo cha kubakiza wadudu shambani.
Alisema tatizo jingine ni baadhi ya wakulima kupiga dawa wakati wa jua kali au kipindi mvua inapokaribia kunyesha na kusababisha dawa kuathirika na kuwafanya wadudu kuendelea kuwepo.
Naye Mtafiti wa Kilimo Taasisi ya Utafiti Ukiriguru Epafania Temu alisema wakulima wakitaka kufanikiwa ni vema wakajenga tabia ya kukagua kukagua mazao yao kila mara kwa mara ili wawe kuona kama kuna wadudu wapige dawa au watafute ushauri wa wataalamu.
Alisema ukaguzi wa shamba unatakiwa ufanyike kuanzia mimea inapokuwa midogo na kuendelea na kuongeza wanapoona dosari watoe taarifa haraka na sio kungoja mpaka wadudu wawe wengi ndio watoe taarifa au wapige dawa ya kuua wadudu.
Mtafiti huyo alisema kuwa sio wadudu wote wanaonekana katika pamba ni waharibifu wapo ambao ni rafiki wa pamba ambao kazi yao ni kuwashambulia wadudu waharibifu.
Post a Comment