Ads

Mtandao wanafunzi nchini ( TSNP) kufungua kesi Mahakamani Mauaji ya Akwilina.



Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MTANDAO wa wanafunzi nchini ( TSNP) umemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba ajiuzulu, ukidai ameshindwa kulisamia Jeshi la Polisi kufanya kazi kitaaluma na kufuata sheria.

Pia amesema kupitia wanasheria wao na wa taasisi mbalimbali watashirikiana na wazazi na walezi wa Akwilina Akwilini kufungua kesi ya madai (civil case) mahakamani, kutokana na uzembe uliofanywa na askari polisi ili iwe fundisho kwa polisi wengine.


Mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo akizungumza na waandishi wa habari kulaani kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kuzuia maandamano na kupelekea mwanafunzi wa NIT Akwilina na Akwilini kufariki kwa kufyatuliwa risasi.

Hatua hiyo imefuatia baada ya Ijumaa iliyopita mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Akwilina Akwilini kupigwa  risasi ya moto akiwa ndani ya daladala na sasa imeacha sintofahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo, amesema matukio kama hayo yamekuwa yakishamiri siku hadi siku nchini.

"Ikiwa yote haya yanatokea, hatujaona wala kusiki kauli ya waziri wa mambo ya ndani juu ya mambo haya zaidi ya kuagiza uchunguzi ufanyike, ambapo kimsingi Tanzania tumekuwa na chunguzi nyingi zinazoendelea na hadi sasa hazina majibu,"

"Hivyo basi, sisi hatuamini kama uchunguzi pekee ndio utakuwa chachu ya kukomesha matendo haya  yanayoendelea kutokea na kufanya raia tukiwemo sisi wanafunzi, kuishi kwa hofu bila kuwa na uhakika na usalama wetu. Cha msingi tunamuomba kwa heshima na taadhima waziri Dk. Nchemba ajiuzulu kwa hiari yake," amesma Nondo.

Amesema huo utakuwa ni mwanzo mkubwa wa kukaribisha mabadiliko katika jeshi la polisi na kwamba kuondoka mkuu kwa makosa ambayo hakutenda, itarekebisha utendaji.

Nondo ameomba Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa waziri huyo ikiwa atashindwa kujiuzulu kwa hiari yake.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti Hugo wa TSNP ametaka hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya askari polisi waliotenda unyama huo wa kukatisha haki ya kusoma pamoja na haki ya kuishi kwa mwanafunzi mwenzao, lakini pia kwa kukiuka sheria na maadili ya kazi yao katika kulinda amani ya raia.

Pia amelitaka jeshi hilo likiongozwa na IGP Simon Sirro lijitathimini upya na kujipima namna linavyotenda kazi zake na kama kweli lipo kawa ajili ya kulinda usalama wa  raia au la!

No comments