Ads

Dkt, Mndolwa awataka wadau kufuata haya ili kuisaidia nchi ya Tanzania katika suala la maadili hususani (Mavazi)


Mwambawahabari
WADAU mbalimbali nchini wakiwemo Wazazi,Taasisi za dini  pamoja na Wizara wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kusimamia suala la maadili kwa vijana husani katika mavazi pamoja na kueka sheria ambayo itaweza kumuwajibisha mtu endapo atakwenda kinyume na utamaduni wa nchi ya Tanzania.

Rai hiyo, imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi kupiti chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Edmund Mndolwa alipokuwa katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kufatia Tamko lililotolewa na Rais John Magufuli katika kusimamia suala la mavazi.

Amesema kuwa, katika suala la maadili hususani upande wa mavazi kwa nchi ya Tanzania bado lipo katika sehemu mbaya kutokana na wazazi kukosa muda wa kukaa na watoto wao na kuwafundisha maadili mazuri ambayo yanaendana na jamii, huku akiwataka watalii wanaofika nchini humo kufuata maadili ya nchi.

"Nataka niseme ukweli kwa nchi yetu ya Tanzania suala la maadili bado tuko nyuma sana, Vijana wanavaa nguo za ajabu sana hazirishi kwa kweli, mimi naona imefika mahala kila mtu ajitolee kwa nafasi yake kulisimamia suala hili ili tupate jamii yenye maadili mazuri kwa vizazi vijavo kwani tatizo hili limeathiri kila rika" amesema Dkt Mndolwa.

Aidha amesema kuwa, katika kupambana na. tatizo hilo wao kama Chama wameweka mikakati ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu katika kuhakikisha kuwa wanatimiza na kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt, John Magufuli la kuwataka wasimamie maadili na mavazi yenye staha mbele ya jamii.

Ameongeza kuwa mikakati ambayo wameshajiwekea ni pamoja na kuielimisha jamii pamoja na kuhakikisha kuwa shule zote 55 walizo nazo zinakua na walimu wa kusimamia maadili na kuhakikisha maadili ya shule ni mazuri na tutakuwa na vigezo vya kuwapima.

"Tunataka baadae tuzungumze na wizara ya elimu ili  huko mbele ya safari tukaweza kuweka somo ya maadili katika mtaala na kuweza kufundishwa katika mashule yetu yote hapa nchini ili kususdi jamii,iweze kuelewa umuhimu wa kuwa na maadili bora ndani ya jamii" amesema Mndolwa.

No comments