Ads

DC MJEMA ATOA WOSIA MZITO KWA WASICHANA








Girl Guides (Wasichana) wote Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa na jamii kwa kujiepusha na vishawishi vya wanaume na kuleta utofauti shuleni kwa kusoma kwa bidii ili wajenzi kuisaidia Taifa kuwa na wasomaji wenye maadili.
 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe Sophia Mjema alipokuwa akizungumza katika  katika sherehe ya kuanzishwa kwa chama cha Girl Guide kilicho ndani ya chama cha Scout, na kuwataka  wasichana hao kuwahamasisha wasichana kwa wingi kujiunga katika chama hicho ili kuwajengea  tabia njema wasichana.
 Aidha amewataka  wakufunzi wote kuenda katika mashule kuwafundisha watoto wa kike na kuwasaidia kuwapa mafunzo yatakayo wa saidia katika maisha  kujitambua wakiwa katika umri wa usichana.

"Maadili yanatengenezwa na sisi kama wanawake tunalojukumu la Kuya jenga maadili na maadili yakiwa promoka tuta ulizwa tulikuwa wapi? naomba kilamsichana ashirikishwe katika chama hiki, kimesaidia Sana na viongozi wengi wanawake walipata chama hiki na leo tunashuhudia ni wamekuwa mfano bora kwa jamii" Alisema.

Waanzilishi wa Chama hiki waliona vijana wa kike  na wa kiumeni wananyanyasika  walikuwa mke na Mume mke , Mke akaanzisha Girl Guide na Mume akaanzisha Scout, na vyama hivi vime saidia Sana watoto na vime wa jenga kimwili, kiakili na kujiamini  na kutenda  mambo mema.
 Hata hivyo amewataka na wazazi na walezi kuangalia mienendo ya watoto wao ili kujenga Taifa imara lenye watu wenye maadili mema wanaojitambua hasa wanawake na kusema  kuwa kufanya hivyo kuta wasaidia kupunguza mimba mashuleni na kupunguza wimbi la watoto wa mitaani  na kusaidia kupata wasomi watakao saidia Tanzania  ya viwanda.

"Tuna hitaji wasomi hasa wanasayansi wasichana wetu nao tunataka wasome ili waweze wataalam Tanzania yetu I nahitaji wataalam wengi na Rais wetu ametoa elimu bure naomba tuitumie vizuri kwa kuwa elimisha watoto wetu ili nao wajenzi kuwa wazazi bora watakao Saidi familia zao"Alisema.

Kwa upande wake mmoja wa waasisi wa chama hicho nchini Bibi Faith Mwasala , amewataka watoto wakati Kike kujiamini na kutoonyesha udharifu wao kwa Wanaume na kuacha kuendekeza njaa na tamaa ya feha














No comments