DC KILWA AAPA KUENDELEA KULA SAHANI MOJA NA WAVUVI HARAMU.
Mwambawahabari
Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Christopher Ngibiagai ameapa kuendelea kupambana na uvuvi haramu wilayani humo ili kuongeza mapato ya halmshauri ya wilaya hiyo na serikali kuu.
Ngubiagai alitoa ahadi hiyo mjini Kilwa Masoko, mbele ya wadau mbalimbali na wanavikundi wa vikundi vya ulinzi shirikishi na usimamizi wa rasilimali za bahari (BMU), Alipozungumza nao kuhusu mikakati na haja ya kuimarisha, kuendeleza na kianzisha vikundi shirikishi vya ulinzi na usimanizi wa rasilimali za bahari wilayani humo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema ni jambo lisilokubalika kuona wavuvi haramu wakififisha juhudi za serikali za kulinda, kutunza na kuendeleza maliasili na rasilimali za nchi. Wakati yeye nisehemu ya viongozi wa serikali hiyo ambao waliapa kuitumikia na kuwatumikia wananchi kwa moyo wote.
Ngubiagai akiwa katika hali iliyoonesha anakerwa na kuchukizwa na vitendo vya wavuvi haramu, alisema nijambo lisilokubalika wala kuingia akilini kwa mwenye uwezo wa kufkiri, wilaya ambayo inamaliasili nyingi, ikiwamo bahari yenye kilometa za mraba 1221 kuwa nyuma kiuchumi.
“Niwakati sasa kwetu sote,yaani viongozi, wananchi na wadau wamaendeleo ikiwamo WWF tushikamane katika kulinda,kuendeleza na kianzisha vindi vingi zaidi, kwa upande wangu naawaapiza sitachoka kupambana nao hadi ushindi kamili upatikane, "alisisitiza.
Alizitaja baadhi ya faida zinazopatikana nazitakazo patikana baada ya kuiweka bahari kwenye mikono salama kuwa ni kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, kurithisha maliasjli kwa vizazi vijavyo na kuongezeka kwa samaki baharini.
"Tunatambua kwamba uvuvi ni sekta ya pili inayoingizia mapato kwa wingi halmshauri yetu baada ya sekta ya kilimo. Lakini hata serikali kuu inapata kodi, kwahiyo hatuna budi kushirikiana, nakila mmoja atimize wajibu wake kwa nafasi yake,"alisisitiza Ngubigai.
Miongoni mwa wilaya zinazokabiliwa na uvuvi haramu ni wilaya ya Kilwa Hata hivyo kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya,tangu kuanzishwa vikundi hivyo na doria zinazofanywa mara kwa mara zimesababisha kasi ya uvuvi haramu kupungua. Huku kiwango cha upatikani samaki kikiongezeka kwa kasi pia.
Post a Comment