Waziri Mwakyembe:NIC Rudisheni Pesa za Nyumba Mlizowauzia BAKITA.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maagizo kwa Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi
(kulia) kulitaka Shirika la Bima La Taifa (NIC) kurejesha fedha za
nyumba walizowauzia kwa matumizi ya ofisi kutokana na Shirika hilo
kushindwa kuwatoa wapangaji wake katika nyumba hizo huku kukiendelea
kuwa na mgogoro leo tarehe 15/08/2017 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi akimwonyesha Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa
kwanza kulia) moja ya nyumba anayoisha mpangaji aliyegoma kuhama katika
nyumba hizo ambazo zimekwishauzwa kwa baraza hilo leo jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Seleman Sewangi akimweleza Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Mchezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo
pichani) namna mradi wa Kongoo wanaouandaa unavyofanya kazi na
utakavyosaidia mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa kutumia kompyuta
katika ofisi za baraza hilo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ( wa kwanza kushoto) akimzungumza
na mtafsiri wa Lugha ya Kiarabu Bw.Shawwaal Marinda wa Baraza la
Kiswahili la Taifa (wa kwanza kulia) alipotembelea taasisi hiyo leo
jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Mchezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ( kushoto ) akiwaonyesha waandishi
wa habari moja ya kitabu cha kujifunza Kiswahili alichopewa kama
zawadi na Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.
Seleman Sewangi (kulia) leo jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi
zao.
………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM
15/08/2017
Dar es Salaam.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) la
agizwa kurejesha pesa za nyumba walizowauzia Baraza la Kiswahili la
Taifa (BAKITA) kwa matumizi ya ofisi zilizokuwa na gharama ya kiasi cha
shilingi bilioni 1.5 pamoja na riba.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi hizo za BAKITA kwa lengo
la kufuatilia maendeleo ya baraza hilo pamoja na kutaka kufahamu namna
wanavyofanya kazi.
“Kama Shirika la Bima la Taifa
limeshindwa kuwaondoa wapangaji wake wakati serikali imeshakwisha
kukamilisha malipo yote basi hakuna haja ya kuendelea kusumbuana ni
vyema warejeshe pesa hizo ili Baraza litafute sehemu nyingine ya
kununua majengo mengine ya ofisi”, alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Pamoja na hayo naye Katibu
Mtendaji wa BAKITA Dkt.Seleman Sewangi alieleza kuwa malipo ya nyumba
hizo walizonunua kutoka NIC kwa ajili ya matumizi ya ofisi
yalishakamilika tangu mwaka 2014 lakini baadhi ya wapangaji waligoma
kuhama katika nyumba hizo ambao walikuwa watumishi wa shirika hilo .
Akiendelea kuzungumza katika ziara
hiyo Waziri Mwakyembe amelitaka Baraza kuwa wabunifu na kufanya kazi
kwa bidii ya kutangaza na kukuza lugha ya Kiswahili kwani taasisi hiyo
ndiyo yenye dhamana ya kutangaza lugha hiyo nje na ndani ya mipaka ya
nchi.
“Lugha ya Kiswahili inakuwa kwa
kasi kubwa kwani tayari Umoja wa Afrika umeshaazimia kuanza kutumia
lugha hiyo katika mikutano yake hivyo ni vyema kuongeza jitihada za
kutengeneza mifumo thabiti itakayo rahisisha usambaaji wa lugha
hii”,aliongezea Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Pamoja na hayo naye Katibu
Mtendaji wa BAKITA Dkt. Selemani Sewangi alimweleza Mhe.Waziri kuwa
kwa sasa Baraza linafanya Mradi wa Kongoo (Kopasi) wenye lengo la
kukusanya matini zenye jumla ya maneno milioni hamsini ambazo zitakuwa
chanzo muhimu cha data za kamusi na utafiti wa Kiswahili pamoja na
ufundishaji wa lugha hiyo kwa kutumia kompyuta.
Post a Comment