Mtoto Aliyeungua Mikono Sasa Kurejea Darasani
Mwambawahabari
Mtoto
aliyeungua na kushindwa kuendelea na masomo mkoani Mtwara ametibiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na sasa anaweza kuendelea na
masomo pamoja na kufanya shughuli zake za kawaida.
Mtoto
huyo aliungua moto baada ya kusukumwa na mwenzake shuleni na hivyo
kuungua mikono yote miwili na kusababisha vidole kujikunja na
kushikamana.
Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari bingwa walifanyia upasuaji na sasa amepona.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji, Ibrahimu Mkoma amesema mtoto Mwanahidi Hamisi
aliungua miaka saba iliyopita na mikono yake kuadhirika na kushindwa
kufanya kazi yoyote.
Amesema
mwaka 2015 mtoto huyo alifanyiwa upasuaji mkono wake wa kulia katika
Hospitali ya CCBRT na kwamba sasa anaendelea vizuri.
Dk
Mkoma amesema Juni 7, 2017 Muhimbili ilimpokea mtoto huyo na baada ya
kufanyia uchunguzi walimfanyia upasuaji mkono wa kushoto na kunyoosha
viungo katika vidole vyake ambavyo vilikuwa vimejikunja.
“Baada
ya kuungua moto vidole vyake vilishikana na viungo kujikunja, lakini
tumefanikiwa kuvinyoosha viungo hivyo na sasa Mwanahidi anaendelea
vizuri na matibabu,” amesema Dk Mkoma.
Amesema
mtoto huyo sasa anaweza kufanya kazi mbalimbali kama kufua na kwamba
anaweza kundelea na shule tofauti na awali baada ya kuungua.
Mama wa mtoto huyo, Amina Mohamed Mkadengile ameambiwa kwamba anapaswa kumfanyia mazoezi mtoto wake ili aimarike zaidi.
“Daktari
amenielekeza jinsi ya kumfanyia mtoto mazoezi, nitakuwa nafanyia
mazoezi katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Nawashukuru
sana madaktari wa Muhimbili na wauguzi kwa kunipatia huduma nzuri,”
amesema mama wa mtoto huyo.
Post a Comment