KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA PAC NA LAAC ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA.
Mwambawahabari
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Mussa Mbaruku akizungumza jambo pale kamati hiyo ilipokutana na viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati kuhusu hesabu za fedha za Taasisi husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma. kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Juma Aweso
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akiongoza kikao cha kamati hiyo pale ilipokutana na viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati kuhusu hesabu za fedha za Taasisi husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia mazungumzo baina yao na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi lengo likiwa ni kupitia Mahesabu na Maagizo ya kamati hiyo, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Naghenjwa kaboyoka(katikati).
Post a Comment