MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA, AWATAKA WAZAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUSHIRIKIANA NA KAMATI ZA SHULE ILI KUONGEZA UFAULU WA WANAFUNZI.
Na John Luhende
mwambawahabari
Meya wa jiji la Dar es salaam , Isaya Mwita Charles amewataka Wazazi wote wa jijini Dar es salaam kushirikiana na kamati za shule ili kutatua tatizo la kufeli kwa wanafunzi katika shule za serikali Mkoani humo.
Akizungumza katika ibada ya juma Pili na waumini wa Kanisa la Ufunuo lina lo ongozwa na Nabii Bendera lililopo Kimara Bonyokwa jijini Dar es salaam amesema ili kuongeza ufaulu kwa shule hizo nilazima wazazi waunangane kwa pamoja na kamati za shule ikiwa ni pamoja na wazazi mmoja mmoja kufuatilia Maendeleo ya shule kwa watoto wao .
" Ndugu zangu tusipo shirikiana katika
jambo hilo tutakuwa wa mwisho kila siku Sasa tubadilike ili kunusuru watoto wetu" alisema
Pia ni jambo la msingi kama tukishirikiana kuwa pata walimu penye upungufu wa masomo husika tusingoje tu serikali ituletee walimu wazazi wanaweza kujipanga wakalipia hata walimu , walimu niwengi wapo mtaani hawana kazi.
jambo hilo tutakuwa wa mwisho kila siku Sasa tubadilike ili kunusuru watoto wetu" alisema
Pia ni jambo la msingi kama tukishirikiana kuwa pata walimu penye upungufu wa masomo husika tusingoje tu serikali ituletee walimu wazazi wanaweza kujipanga wakalipia hata walimu , walimu niwengi wapo mtaani hawana kazi.
Kauli ya Meya imekuja baada ya shule za Mkoa huo kutofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ambapo shule za mwisho zimetoka Mkoa humo.
Aidha amewataka wauminihao na watanzania kuiombea nchi na viongozi wake ili Tanzania iendelee kuwa na amani,na watu wake waendelee kuishi kama ndugu bila kujali tofauti zao za dini, kabila na kisiasa.
Amesema ili Dunia iendelee kuwa na amani nilazima Ma Taifa la Marekani liwe na amani , Taifa hilo likiyumba dunia yote itatetereka kiuchumi na kuwataka watanzania kuimbea Marekani na Rais wake ili waendelee kuzi saidia nchi za Afrika.
"Marekani ikisitisha misaada yote Afrika sijui itakuwaje Tumwombee na Trump"
Naye kiongozi wa Kanisa la ufunuo Nabii John Bendera amemshukuru Mhe Isaya kujumuika katika ibada ya jumapili na kumwombea Baraka na kutabiria makubwa katika kazi zake.
Post a Comment