SHULE YA KSIJ ALMUNTANZIR YAMKABIDHI MADAWATI MKUU WA MKOA WA DAR MH.PAUL MAKONDA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akikata utepe kwenye hafla ya kukabidhiwa wadawati leo jijini Dar es Salaam.
Shule za Almuntazir zimekabidhi madawati kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda kwa kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.John Pombe Magufuli.
Akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu KSIJ ambayo inazisimamia shule za Almuntazir Imtiaz Laiji,amesema kuwa wanaungana na Rais Magufuli kusaidia juhudi zake katika sekta ya elimu na pia wanampongeza Paul Makonda kwa kuendeleza na kampeni zake za kuchangia madawati kwa shule zote za Dar es salaam.
“Kwa kweli tunampongeza sana Rais Magufuli kwa juhudi zake katika sekta ya Elimu kwani ameleta mapinduzi makubwa kwa kutoa Elimu bure pamoja na kutaka shule binafasi zipungunze gharama ya ada zao ili kuendana na vitenga uchumi kwa wananchi walio katika hali duni ya kimaisha”alisema Laiji
Hata hivyo amesema kuwa ilikuwa ni aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania yenye misitu Mikubwa ambayo inaweza kusafirishwa magogo nje ya nchi huku ikiwaacha watoto wakisota kwenye sakafu za vumbi katika mbio za kutafuta Elimu.
Almuntazir ni shule kongwe na zina historia ndefu ya miaka ya zaidi ya arobaini na shule ya kwanza kuanzishwa ilikuwa ni ya Chekechea na ilianza na wanafunzi wasiozidi 150 mwaka 1975 hadi mpaka sasa jumla ya shule za Almuntazir zilizopo ni sita na wanafunzi zaidi ya 4500,walimu pamoja na wafanyakazi zaidi ya 500.
“Shule hizi zinamilikiwa na taasisi ya dini,udini na ubaguzi haupo katika shule hizi kwani tuna wanafunzi wa madhehebu wa dini zote wanaruhusiwa kusoma katika shule hizi”alisema Laiji
“Shule hizi zinamilikiwa na taasisi ya dini,udini na ubaguzi haupo katika shule hizi kwani tuna wanafunzi wa madhehebu wa dini zote wanaruhusiwa kusoma katika shule hizi”alisema Laiji
Katika upande wa elimu shule imejipanua kiasi cha kupigiwa mfano,maana ni shule ya mwanzo isiyo ya Serikali ambayo imeanzisha kitengo cha kufundisha watoto wenye ulemavu na ushonaji jumla ina wanafunzi 80 pamoja na kuwa na walimu waliobobea vilivyo jinsi ya kuwafundisha watoto hao.
Licha ya hayo kuna matatizo yanayoletwa kwa makusudi ili kuvuruga jitahidi hizo kwani siku za karibuni limetokea kundi la wazazi wachache ambao wanajiita ni Umoja wa Wazazi wenye watoto katika shule za Almuntazir na kujaribu kuchafua jina la shule hizo.
Almuntazir kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Mh.John Pombe Magufuli na juhudi zako binafsi za kuwapatia mazingira bora ya kujifunza kwa kila mtoto tumeamua kukukabidhi mchango mdogo wa madawati 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20.
Kwa upande wa mgeni Rasmi amesema kuwa anapongeza juhudi zilizooneshwa na Almuntazir kwa kuchangia madawati kwa mkoa wa Dar es salaam pamoja na kuungana kumsapoti Rais Magufuli kwa utendaji kazi wake wa awamu ya tano kwani kwa mwaka mmoja aliokaa madarakani ameweza kuinua na kuziba minya ya utumiaji ovyo wa fedha za umma.
“Hii ni hatua kubwa kwenu kwa kuamua kujitolea na kununua madawati hayo kwa mapenzi yenu kwa watoto ambao walikuwa wanakaa chini hakika mnasitahiri pongezi kubwa mno kiukweli sina cha kuwapa zaidi nawaombea mafaniko mema katika kuinua elimu hapa nchini”alisema Makonda
Sherehe hizo za kukabidhi madawati kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda pia zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali Shehe wa mkoa Sheikh Musa Salum Hadi,mwenyekiti wa KSIJ DSM AZzim Dewji,Makamu wa mwenyekiti wa Jumuiya ya KSIJ DSM Riyaz Bhojani,waheshimiwa wajumbe na viongozi wa jumuiya ya KSIJ DSM pamoja na wajumbe wa CBE,na Mshauri wa Elimu katika shule za Almuntazir Mh.Philipo Mulugo (MB) wa jimbo la Songwe na ni mlezi wa shule za Almuntazir.

Post a Comment