Ads

PPF YADHAMINI WIKI YA USALAMA BARABARANI




Mwambawahabari
Mfuko wa Pensheni wa PPF utashiriki katika Wiki ya Usalama Barabarani ambayo utafanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 7 hadi 11 Novemba, 2016.

Meneja Uhusiano wa mfuko wa PPF, Lulu Mengele alisema kuwa mfuko huo umeamua kuunga mkono suala hilo kwakuwa ni la msingi litakalotoa elimu kwa makundi husika ili kuepusha ajali na kuhakisha usalama wao katika kujenga uchumi wa nchi.

Pia Mengele alisema mfuko wa PPF unatambua umuhimu wa makundi hayo na kwamba umeanzisha Mfumo wa Wote Scheme ukiwa na lengo la kuboresha maisha ya wanachama waliojiajiri

“kupitia mfumo wa ' wote Scheme' mwanachama atakuwa na uhakika wa kupata bima ya afya,  mkopo wa elimu,na kupata mafao ya pensheni ya uzeeni pindi anapotimiza miaka 55" amesema

Hata hivyo alisema mfuko huo unatoa wito kwa washiriki wote na jamii kwa ujumla kujiunga na mfuko wa wrote scheme ili waweze kufaidika na huduma zinazotolewa.

No comments