Ads

MOTO WAZUA TAHARUKI KUBWA BANDARINI DAR ,TPA YASEMA ULIKUWA WA KUTENGENEZWA


Moto ukiwaka kwkasi katika makontena kabla ya vikosi vya zimamoto havija fika kuuzima moto huo, picha zote na John Luhende
Na John Luhende 
mwambawahabari
Taharuki kubwa imewakumba wafanyakazi  wa mamlaka ya bandari Tanzania TPA Mara baada ya motomkubwa kuzuka Leo Majira ya mcha na katika makontena matatu Yaliyojiri dhaniwa kuwa na mzigo wa magurudumu ya gari .



Kamera ya Mwambawahabari  imenasa tukio zima huku wa watu tu walio nusurika katika ajali hiyo wako kimbizwa hospitality mbali mbali za jijini la Dar  es salaam ili kunusuru maishayao.

Akizungumza Mara baada ya moto huo kuzimwa na vikosi vya zima moto vya Bandari na vya makampuni binafsi Afisa  habari wa mamlaka hiyo Peter Milanzi amesema  Motohuo uliandaliwa makusudi ili kupima uwezo wa vikosi vya zima moto kama tukio la ukweli likitokea vina weza kukabili janga hilo.


"Ndugu waandishi mtuwie radhi,
tulilazimika kuto waarifu kuhusu zoezi hili maana yawezekana msinge lichukilia umuhimu tu nashukuru zoezi lime enda vizuri vikosi vyetu vimewahi eneo la tukio na kuuzima moto,nizoezi ambalo huwa tunalifanya kila mwaka" alisema milanzi.




Kwa upande wao wafanya Kazi wa bandari hiyo na Wateja waliofika bandarini kupata Huduma hawakujua kinachoendelea walijikuta katika wakati mgumu kutokana na hali ilivyo kuwa, moto mkali Moshi mweusi mzito ulionekaka kutanda eneo hilo na baadhi yao walianza kukimbia hivyo  huku baadhi ya wana wake wakiangua kilio.




Mkuu wa kikosi cha zimamoto cha bandari hiyo bwana Musa Biboze  alivipongeza vikosi vya vyote vilivyo shiriki zoezi hilo kwa umahili Mkubwa  walivyo zima moto huo mkali wa magurudumu na Mbao,pamoja na magari ya wagonjwa yaliwahi kuwa kubeba majeruhi hao.





No comments