Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) kutokana na kukiuka masharti ya dhamana ya kesi yake,
Lissu anatuhumiwa pamoja na Jabir Idrissa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la MAWIO na Simon Mkina Mhariri wa gazeti hilo na Ismail Merhaboob Meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint kwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la MAWIO.
Leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu, kesi hiyo ilitajwa ambapo mtuhumiwa namba nne hakutokea mahakamani hapo, Mdhamini wa (Lissu) Robart Katula amefika mbele ya Hakimu Simba ambapo amedai kuwa mdhamana wake alimpa taarifa ya kuwa yupo Mwanza katika kesi.
Patric Mwita wakili wa serikali ameitaka mahakama kumfutia dhamana mtuhuminwa kutokana kwenda kinyume na masharti ya dhamana aliyopewa na mahakama hiyo, Faraja Mangula wakili wa upande wa utetezi amedai kuwa mteja wake ameenda Mwanza kusimamia kesi za uchaguzi.
Baada kusikiliza pande zote Hakimu Simba amesema kuwa mtuhumiwa huyo ameondoka bila ya ruhusa ya mahakama, na kueleza kuwa hati ya kukamatwa kwa Lissu itolewe na hakutakuwa msamaha , pia wadhamni wafike mahakamani hapo kueleza mdamana wao wameenda kinyume na masharti ya dhamana.
Hakimu Simba amesema kuwa dhamana kwa watuhumiwa wengine inaendelea,kesi hiyo itatajwa tena tarehe 21 Novemba Mwaka huu.
Post a Comment