Ads

JK : VIJANA TUMIENI FURSA YA MICHEZO KUKUZA VIPAJI


Rais mstaafu wa awamu ya NNE wa jamhuri ya muungano wa Tanzania   mh .Dr Jakaya Kikwete  katikakati aliye vaa shati  ya mistari walioko kulia na kushoto ni wakufunzi wa NBA kutoka nchini Marekani,na aliye vaa fulana ya kijani nimwakilishi wa mmiliki wa kituo cha  michezo cha Jakaya kampuni ya simbion,(picha zote na John Luhende)

Na Maria Kaira Dar
Mwambawahabari
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dr. Jakaya Kikwete amewataka vijana kutumia vizuri fursa za michezo zinazojitokeza hapa nchini ikiwa na lengo la kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Aliyasema hayo jijini hapa katika sherehe za ligi ya NBA yaliyoanza kutimua vyumbi  Febuari mwaka huu na kuudhuliwa na Rais wa Toronto Raptors Masai Ujiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Symbion Power Paul Hinks na bingwa wa NBA ya wanawake kutoka timu ya Los Angeles Sparks, Alana Beard.



Pia Dr. Kikwete akazipongeza timu zote za vijana zilizoweza kushiriki katika michuano hiyo huku akizisisitizia umuhimu wa kutumia fursa hizo zinazojitokeza na kuwataka wazazi wasisite kuwapeleka watoto wao katika michezo ili kuweza kujipatia manufaa yao na taifa kwa ujumla katika siku zao za usoni.

"Tayari vijana 50 elfu wameshapita katika kituo hiki cha vijana cha Jakaya Kikwete (JMK park) naamini vijana hao watakuwa wamejifunza na watakuwa wachezaji wazuri hapa nchini na kuwa mfano katika nchi za Nje, pia kwa uwekezaji huu wa vijana kwenye michezo naamini Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu katika mpira wa kikapu kwa kufanya vizuri na kupata wachezaji wakubwa" alisema




Mkufunzi wa mpira wa kikapu Bahati Mbunda ameiomba familia ya mpira wa kikapu kuendelea na moto huo waliouanzisha na kuwanoa vijana katika mchezo huo ili wawe wa mfano na kuweza kuendeleza vipaji vyao siku zote maishani mwao.

"Mwaka kesho tutakua na ligi kama hii ya wasichana naamini utakuwa utamaduni mpya tunaouingiza kwenye jamii ya Tanzania tunaona ligi tuliianza taratibu ila siku zinavyozidi kuendelea tunaona viwango vinabadirika" alisema



Aidha alisema ligi za michuano hiyo NBA zitakuwa endelevu hapa nchini ikiwa na lengo la kuwakuza vipaji vya vijana hao wakiwa wadogo ili wasiweze kuishia njiani.

Hata hivyo mwanafunzi kutoka Shule ya Msingi Tusiime Avelison Bahati alisema anawashukuru waandaaji wa michuano hiyo na kuuomba uongozi kuyafanya michuano hiyo kuwa endelevu ili kuweza kukuza vipaji vyao, pia akawahasa Vijana wenzake kuchangamkia fursa zitakazojitokeza katika michezo 

No comments