HABARI PICHA ,KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA KAMATI YA TAIFA YA URATIBU WA MAAFA NCHINI.
Mwambawahabari
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akifungua Mkutano wa Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa Nchini uliofanyika Novemba 04, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa Nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa mkutano wao kujadili masuala ya Menejimenti ya maafa Novemba 04, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi. Tumpe Mwaijande akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa Nchini uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwapitisha wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa juu ya Mkakati wa Mawasiliano katika kukabiliana na maafa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akichangia hoja kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa wakati wa Mkutano wa Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa uliofanyika Novemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)





Post a Comment