Ads

DC MJEMA ATENGA MITAA YAKUFANYIA BIASHARA WAMACHINGA


Na Rayusa Yasini 

Mwambawahabari

Kufuatia Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wasibuguziwe na watafutiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameenza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo.

Akizungumza  katika ziara yake ya kuzungukia masoko ambayo wanataraji kuwahamishia machinga hao DC Mjema ameeleza kuwa soko la Kivule na Kerezange kwasasa yapo tayari huku akiahidi kushughulikiwa kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi ambapo amewahakikishia uwepo wa ‘route’ za daladala, huku soko la Tabata Muslim likiwa katika hatua za mwisho mpaka mwezi wa 12 masoko yote yatakuwa katika mazingira rafiki.

Pia DC Mjema amezitaja barabara ambazo zitatumika na machinga kwa ajili ya kufanya biashara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ambapo barabara hizo ni Lumumba na Mkunguni huku muda wa kuanza kufanya biashara hizo ni kuanzia saa sita mchana na eneo hilo linauwezo wa kukaa watu zaidi ya 1800.

Katika hatua nyingine DC Mjema amesimamia uabdikishwaji wa machinga waliokuwa wanafanyabiashara zao kandokando ya barabara za mabasi yaendayo kasi, na kuwataka ambao hawajajiandikisha wajiandikishe mapema ili wapatiwe maeneo rasmi.

No comments