RAIS MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI BUKOBA
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Erasto Aron Mfugale kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stephen Makonda ambae uteuzi wake ulitenguliwa na Mhe. Rais tarehe 27.9. 2016.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe kwa Vyombo vya Habari imeeleza kuwa kabla ya Uteuzi huo wa Bw. Erasto Mfugale alikuwa Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya mji wa Masasi.
Uteuzi wa Bw. Mfugale unaanza mara moja.
Post a Comment