Ads

MAMA JANETH: JITOKEZENI KUWASAIDIA WAZEE.


Displaying 11.jpg
NA ; HASSAN SILAYO
mwambawahabari
Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.
“Kundi hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.

Pia Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu.
Aidha, Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175, Maharage Kilo 350  na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.
Akiongea wakati akimkaribisha Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Naye Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.

No comments