Ads

CHANGAMOTO ZA MAADILI YA UONGOZI NA AZIMIO LA ARUSHA KUJADILIWA OCTOBA 14




Na Maria Kaira,Dar
Mwambawahabari
Ikiwa maadili ya uongozi nchini bado ni changamoto wanazuoni wanatarajia kukutana na kujadili miiko ya uongozi na azimio la Arusha Octoba 14 katika ukumbi wa chuo cha kumbukumbu cha mwalimu Nyerere ili kuweza kuwakumbusha wajibu wao katika jamii.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es salaam Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema wameandaa kongamono kwa lengo la kumhenzi hayati mwalimu Nyerere na kuchambua mada mbalimbali walizozichagua siku hiyo.

Profesa Mwakalila amesema kuwa kongamano hilo litafanyika siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Miiko ya uongozi na Azimio la Arusha”pia wananchi wataweza kujua kinachoendelea katika azimio la Arusha.

Aidha amesema maadili basi yanachangamoto kwa kulitambua hilo wamewaarika wanazuoni watano ambao wayaweza kuchambua mada ya Azimio la Arusha na maadili ya uongozi.

“Tumemwalika Dkt Harun Kondo atakaye chambua Azimio la Arusha, Wilson Mkama na Mzee Joseph Butiku watachambua Miiko ya uongozi pamoja na Ibrahim Kaduma na Mhe Philip Mangula watakaojadili maadili ya viongozi,” amesema Prof. Mwakalila.

Hats hivyo  Prof. Mwakalila amesema kuwa Miiko ya uongozi na maadili ya viongozi wa Umma ilisisitizwa na Mwalimu mara baada ya Uhuru na baadaye kusisitizwa zaidi katika Azimio la Arusha la mwaka 1967.

Anna John ni mmoja wa wananchi ameelezea umuhimu wa kongamano hilo kuwa wamefanya kitu kizuri ambacho kitaweza kuwakumbusha viongozi waliojisahau katika uongozi wao na kuweza kukumbuka alichokuwa anakisisitiza hayati mwalimu nyerere katika enzi yake.

" Naimani wanazuoni hao watatukumbusha mengi ili tuweze kukumbuka yale yaliyosaaulika"amesema

No comments