WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 36 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BUS LA BM LUBUNGO MIKESO MKOANI MOROGORO
Basi la Kampuni ya BM linavyoonekana baada ya kupata katika eneo la Mikese Mkoani Morogoro chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni mwendo kasi wa Basi hilo uliopelekea kushindwa kusimama.
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne
vibaya baà da ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam
kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori
lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya
barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese,
barabara
kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumzia ajali hiyo,
amesema chanzo ni mwendo kasi na imetokea majira ya saa 3:30 usiku wa
kuamkia leo ikihuhusisha basi la mwisho kutoka jijini Dar es Salaam kwenda
Morogoro, mali ya kampuni ya BM, baada ya dereva wake kufika Lubungo eneo
lenye kona na mteremko mkali, na akiwa mwendo kasi, kukutana mbele na lori
likiwa na tela, likitokea uelekeo wa Morogoro kuelekea Dar es Salaam, likiwa
linamalizia kupita lori jingine lililokuwa limeegesha barabarani baà da ya
kuharibika, ambapo dereva wa basi aligonga tela la lori hilo lililokuwa kwenye
mwendo na kukosa uelekeo na kupindukia bondeni na kusababisha vifo na
majeruhi hao.
Post a Comment