TRA YAOMBA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WANANCHI
Na Jacquiline Mrisho
mwambawahabariblog
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za Maafisa
wanaofanya kazi kinyume na maadili.
Akizungumza na mwandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu
ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na
kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba wananchi
kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya
maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema
Kayombo.
Mkurugenzi Kayombo
ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu kwa namba
0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516 na
kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa
kazi.
Aidha Kayombo amependa
kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi
atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.
TRA kupitia Idara yake
ya Mambo ya Ndani imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya
watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia uchunguzi na baadhi
ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.
Post a Comment