AHADI ZA KIBONDE ATAKAZOTELELEZA NDANI YA SIKU 100 AKICHAGULIWA KUWA RAIS
Na Angelina Mganga
DAR ES SALAAM
MGOMBEA Urais wa Chama cha Maarifa,KIlimo na Nishati (MAKINI), Coaster Kibonde ametoa ahadi ndani ya siku 100 endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania ataanza na marekebisho ya Katiba kwa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Kibonde ametoa ahadi hiyo Septemba 2,2025 katika Viwanja vya Bakhresa Manzese Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Kitaifa za Chama hicho.
Aidha,amesema kwamba akichaguliwa kuwa rais atahakikisha elimu kuanzia chekechea Hadi chuo kikuu itatolewa Bure pamoja na kuwahakikishia wahitimu wa vyuo vikuu kuwa hawatakuwa na haja tena ya kurejesha mikopo yao serikalini.
"Kijana wa kitanzania akikosa elimu ni Sawa na kumfunga kifungo Cha maisha huku akieleza kuwa hiyo ndio sababu kubwa ya chama hicho kutoa elimu katika ngazi zote kwa gharama za serikali",amesema Kibonde
Pia ameeleza kuwa atatoa ekari Tano za ardhi kwa kila Mtanzania pamoja na hati miliki ili vijana waweze kuaminika kwenye taasisi za fedha.
Sanjari na hayo amesema kwamba atafanya mageuzi makubwa ya kiviwanda na viwanda hivyo vitazalisha Mali zinazohusiana na kilimo ikiwemo pembejeo hivyo pembejeo zitamsubiri mkulima
Hata hivyo, amesema kwamba endapo atachaguliwa atahakikisha viongozi wote wa vyama wagombea wote waliogombea urais atawapatia ajira katika Serikali huku akibainisha kwamba wa kwanza kumuajiri atakuwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mwanadiplomasia mzuri wa kimataifa,kiuchumi amoja na mwanadiplomasia mzuri wa mambo ya kisiasa
Kwa upande wake Mgombea Mweza Azza Haji Suleiman amesisitiza amani,umoja na utulivu pia ametoa wito kwa vijana kuepuka kushawishika kuvuruga amani ya nchi yetu na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kukipigia kura chama cha Makini Oktoba 29,ili kukipatia ushindi
Post a Comment