Ads

WAJASIRIMALI TEMEKE WAHAMASIKA NA MATUMIZI YA MAJIKO YA NISHATI SAFI

Na Goodluck Assenga, Dar es Salaam.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limeshiriki Kongamano la Nishati Safi lililoandaliwa na Mtandao  wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania kwa kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wajasiriamali wadogo zaidi ya 70 wakiwemo Mama Ntilie, Baba Lishe na makundi mengine ya wafanyabiashara wadogo kati ya hao 20 wamejiorodhesha kupata majiko hayo.
Kongamano hili limefanyika leo Agosti 30, 2025  katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Afisa Huduma kwa Wateja, Bw.Goodluck Assenga ameeleza kwamba Umeme ni nishati nafuu zaidi jikoni kwa kutumia vifaa  sahihi vya umeme, kwakuwa nishati hii inaokoa muda jikoni, inatunza mazingira na ni rafiki kwa mtumiaji kwakuwa ni salama
Aidha, wajasiriamali hao walipata kuona kwa vitendo namna majiko hayo yanavyofanya kazi kwa kupika vyakula mbalimbali  kwa urahisi na haraka.
Mgeni rasmi katika kongamano  hilo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Uwezeshaji wanawake Tanzania (TAWEN) Mhe.Janeth Mbene, ambae ameipongeza TANESCO  Temeke kwa juhudi za kuhamasisha matumizi  ya nishati safi ya kupikia.

No comments