WANASIASA WAASWA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU:JAJI MUTUNGI
Na Angelina Mganga
DAR ES SALAAM
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa Kitaifa wa vyama vya siasa kufanya siasa za kistaarabu wakati huu keelekea uchaguzi mkuu .
Haye yamebainishwa Leo Agosti 18,2025 jijini Dar es Salaam na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi wakati akifungua mafunzo kuhusu Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa viongozi hao kwa kusema kwamba wakawe walimu Bora na wasaidizi kwa wagombea na viongozi wa chama kwa ngazi za chini.
Mafunzo hayo yemefanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere(JINCC) Jijini Dar es Salaam ambapo kikao hicho kimeandaliwa kwa siku moja kwa ajili ya viongozi hao mara baada ya hapo kuendelea na ratiba zao za maandalizi ya uchaguzi katika mchakato mzima wa uteuzi wa upatikanaji wa wadhamini.
"Ninatambua kuwa mpo katika mchakato wa uteuzi wa wagombea na kutafuta wadhamini ,kwa hiyo kikao hiki Cha siku Moja ni maandalizi muhimu sana ya uchaguzi",amesema Jaji Mutungi
Aidha ,amesema kwamba vyama vya siasa haviwezi kuepuka kushiriki uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuwa wagombea wote lazima wadhaminiwe na vyama.
Amewataka viongozi hao kutumia mafunzo hayo walioyapata kwa ajili ya kuelimisha wagombea wa chama na mawakala katika ngazi zote kuanzia kata ,wilaya na majimbo.
"Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi,mtafundishwa namna ya kuzingatia kwa ukamilifu matakwa ya Sheria ya gharama za uchaguzi,haya yataweza kuwaongezea uelewa ili kwenda kutekeleza matakwa hayo kisheria",amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Juma Khatibu amesisitiza kwamba viongozi na watendaji wa vyama vya siasa nchini kuzingatia masharti ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ili kuepuka kasoro katika Uchaguzi Mkuu wa.mwaka huu.
Sanjari na hayo Mwenyekiti huyo ameimpongeza msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kuwaleta pamoja viongozi hao qa kitaifa na watendajl wa vyama kwa kuwapatia elimi na kiumarisha msingi wa kidemokrasia
Post a Comment