MARK ISDORY MHEMELA ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MTUMBA
Na mwandishi wetu
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Mjini,Adv.Cosmas Nsemwa ,Agosti 14,2025 alimkabidhi fomu za uteuzi kwa nafasi ya Ubunge,Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Wakulima (AAFP) na Mgombea Ubunge Jimbo la Mtumba Dodoma kupitia Chama cha Wakulima (AAFP ),Mark Isdory Mhemela
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Ubunge umeanza Agosti 14,2025 ambapo unatarajiwa kutamatika Agosti 27,2025 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 29,2029
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Mhemela amesema kwamba nia yangu na dhamira yangu yakugombea nafasi hii ni kwenda kuwatumikia wananchi wa Mtumba pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika maeneo ya Jimbo hilo.
"Nimeamua kwa dhati kutoka moyoni mwangu kwenda kuwatumikia wakazi wa Mtumba na nitahakikisha kutatua changamoto na kuwaletea maendeleo wakazi wa Jimbo hilo",amesema Mhemela
Ameongeza kwamba kwa Nia yangu ya dhati na moyo wa uzalendo kwa chama changu endapo nitachaguliwa nitasimamia Ilani ya Chama kuwaletea wananchi maendeleo na kutafuta fursa mbalimbali zitakazo wapatia wananchi kipato.
Aliendelea kwa kusema kwamba wananchi wa Mtumba watarajie maendeleo makubwa na nitakuwa bega kwa bega na wananchi kutatua shida pamoja na kuwasaidia
Post a Comment